Pre GE2025 Kwanini mnatuandikisha majina ya mpiga kura na hamtoi vitambulisho wala kuchukua picha ya anayejiandikisha?

Pre GE2025 Kwanini mnatuandikisha majina ya mpiga kura na hamtoi vitambulisho wala kuchukua picha ya anayejiandikisha?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Kuna jambo nimejaribu kulitafakari sana kuhusu huu uandikishaji ,miaka yote tunaandikishwa na kupewa vitambulisho.

Ni kwanini awamu hii mnaandika majina tu na hamtoi kitambulisho? Ni nini lengo la tume na kwa wale ambao hawana vitambulisho chaguzi zijazo watafanyaje ?
 
Nadhani vitambulisho vinatolewa kwa wale ambao hawana!
Mimi ninacho cha zamani na tarehe 27 nov.nitakuwa kwenye harakati zangu za kutafutia wanangu mkate!
Nitafuatilia matokeo kwenye TV kushuhudia jinsi Polisi walivyokuwa wanapola masanduku ya kura na kukimbia nayo!
 
Kuna jambo nimejaribu kulitafakari sana kuhusu huu uandikishaji ,miaka yote tunaandikishwa na kupewa vitambulisho.

Nikwanini awamu hii mnaandika majina tu na hamtoi kitambulisho ? Ninini lengo la tume na kwa wale ambao hawana vitambulisho chaguzi zijazo watafanyaje ?
Inawezekana hawana hela za kuchapisha vitambulisho pia labda uchaguzi wa serikali za mitaa wameuchukulia poa
 
Uchaguzi wa serikali za mitaa hauhitaji kadi kupiga kura, cha msingi ni kujiandikisha kwenye daftari, kwenye eneo lako unalo ishi. Kadi hutumika kwenye uchaguzi mkuu, ambao ni mwakani.
 
Kuna jambo nimejaribu kulitafakari sana kuhusu huu uandikishaji ,miaka yote tunaandikishwa na kupewa vitambulisho.

Nikwanini awamu hii mnaandika majina tu na hamtoi kitambulisho ? Ninini lengo la tume na kwa wale ambao hawana vitambulisho chaguzi zijazo watafanyaje ?
miaka ipi uliandikishwa na ukapewa kitambulisho?

na ulijiandikisha kwa sababu gani hata ukapewa kitambulisho au kupigwa picha?

unaelewa kinachoendelea kweli au umehadithiwa tu na rafiki yako gentleman?🤣
 
Kuna jambo nimejaribu kulitafakari sana kuhusu huu uandikishaji ,miaka yote tunaandikishwa na kupewa vitambulisho.

Nikwanini awamu hii mnaandika majina tu na hamtoi kitambulisho ? Ninini lengo la tume na kwa wale ambao hawana vitambulisho chaguzi zijazo watafanyaje ?
Ndo ushapiga kura hivyo
 
Zoezi linaloendelea ni kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa/kijiji, zoezi hili linahusisha wakazi wa eneo husika tu, lengo ni kwa ajili ya UCHAGUZI WA VIONGOZI ( mwenyekiti wa mtaa au kijiji pamoja na vitingoji hapo tar 27.11.2024)
Zoezi hili ni tofauti na lile la uandikishwaji kwa ajili ya uchaguzi MKUU hapo mwakani 2025 ,huko utapewa kitambulisho cha mpiga kura.
 
Nadhani vitambulisho vinatolewa kwa wale ambao hawana!
Mimi ninacho cha zamani na tarehe 27 nov.nitakuwa kwenye harakati zangu za kutafutia wanangu mkate!
Nitafuatilia matokeo kwenye TV kushuhudia jinsi Polisi walivyokuwa wanapola masanduku ya kura na kukimbia nayo!
Ccm wanapenda watu kama wewe
 
CHADEMA HAWATAKI VIJANA WAJIANDIKISHE, JE WANAWAOGOPA KWENYE UCHAGUZI?

Sauti za Chadema sasa zinapaza malalamiko yasiyo na mashiko, wakidai kwamba Tume ya Uchaguzi (NEC) inaandikisha wanafunzi kwa lengo la kuwaandaa kupigia kura CCM. Ukweli ni kwamba, kila kijana mwenye miaka 18 ana haki ya kikatiba kujiandikisha na kupiga kura.

Hii siyo mbinu ya kisiasa bali ni utekelezaji wa sheria, kwani vijana waliozaliwa mwaka 2006, wakiwemo wa umri wa miaka 17 mwaka huu, watafikisha miaka 18 ifikapo mwakani. Je, Chadema wanataka kuwanyima haki zao kikatiba?

Chadema wanatakiwa kuelewa kuwa kila aliyeandikishwa ameonesha kitambulisho kinachoonesha umri wake halali. Kuibua tuhuma za "kuandikisha watoto" bila kutoa ushahidi wa vitambulisho ni mbinu ya kisiasa ya kutengeneza mazingira ya kujiondoa mapema au kutafuta kisingizio endapo watashindwa tena mwakani. Tumeona mbinu kama hizi mara kadhaa—wakishindwa, hukimbilia kusema "tulibambikiwa."

Nani anaweza kuwazuia vijana wenye ari na shauku ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi? Hili si swali la wafuasi wa CCM bali ni ishara ya hofu ndani ya Chadema, wakijua kuwa kizazi cha sasa kinatambua haki zake na hakitadanganywa kirahisi. Wanapojaribu kupinga ushiriki wa vijana, wanaonesha wazi kuwa hawataki sauti za kizazi kipya zisikike.

Kwa kifupi, malalamiko ya Chadema si hoja ya msingi bali mbinu ya kuwatisha vijana na kuwapotezea imani katika mchakato wa uchaguzi. Uchaguzi si mchezo wa kuigiza bali ni nafasi ya kila raia, awe kijana au mzee, kuamua hatma ya taifa kupitia sanduku la kura.

Kama Chadema wana hofu ya kushindwa, basi wanapaswa kujipanga na kuja na sera bora badala ya kutengeneza visingizio visivyo na msingi.
 
Back
Top Bottom