Kwanini mtoto hulia baada ya kuzaliwa?

bway hermit

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2017
Posts
1,337
Reaction score
2,339
Kuna rafiki alinambia kun mambo 5 ambayo humfanya Mtoto kulia...
Yeye alinijuza mawili tu

1: Kufungua mapafu ili Kupitisha hewa

2: Huona mabaya yafanywayo duniani.

Je, sababu zingine zipi?
 
Kuna portion ya moyo inahitajika kufunguka wakati mtoto ametoka kwenye tumbo la uzazi hivyo inahitajika oxygen wakati huo ili ile sehemu ifunguke ndio maana analia ili kuruhusu oxygen nyingi ipite kwenye mapafu na ndio maana huwa unaona asipolia kuna vitu wanafanya ili aweze kulia kifupi hivyo.
 
Mabadiliko ya ghafla ya mazingira/ hali ya hewa kutoka ya joto la nyuzi 37 degrees centigrade ndani ya tumbo la mama yake hadi hali ya baridi na upepo mkali wa dunia yetu, humfanya alie sana. Kitendo cha kulia husababisha avute hewa ya dunia kwa mara ya kwanza na kuyapanua mapafu yake na kuanzisha automatic breathing process.

NB: Akiwa ndani ya tumbo la mama mtoto huwa hali chakula kwa mdomo wala huwa hapumui kwa pua. Mahitaji yake ya chakula na hewa huyapata kwa mama yake kupitia kitovu chake hadi kwenye kondo la mama yake. Hivyo mapafu huwa yame collapse. Akizaliwa akashindwa kulia basi atashindwa kupumua na baada ya dakika chake lazima ataaga dunia.
 
Kama analia ili oxygen ipite kwenye mapafu ni kwa nini asicheke kwa raha zake ili hewa ipite?? Nafikiri anaona ulimwengu wa ajabu tofauti na alivyokua tumboni. Ndio maana watoto wanaona ulimwengu wa roho, wachawi na mambo yao ya ajabu. Aliyecheka wakati wa kuzaliwa ana tatizo, ni kwa nini afurahie mabaya ya duniani??
 
Mkuu we ni doctor
 
Kuna maumivu anapata katika hiyo process ndio maana analia take your time soma anatomy na physiology topic blood circulation utapata majibu yote
 
Pia ukumbuke mtoto anapolia anajikinga na magonjwa ya moyo
 
Ile feeling anayoipata wakati oxygen inapita kwenye mapafu ndo inamfanya alie na sio kwamba analia ili oxygen ipite.

Hilo suala la kuona ulimwengu wa ajabu ni story tu hamna ukweli hapo.
 
Kweli anatomy na physiology utapata majibu ila watoto kama malaika wana uwezo wa kuona vitu ambavyo havionekani, ni imani tu na wala sio jibu.
 
hilo la kulia naona si kubwa, kubwa ni nani kinamfundisha mtoto aliyezaliwa dakika chache tu kwamba akipewa kitu mdomoni lazima avute ni nini? (anyonye); sababu hajui chochote kile wala hajui kwamba kashazaliwa tayari duniani.
 
Kulia na kucheka yote sawa tu, ni makelele
 
mtoa hoja anasema kwa nini mtoto alie na asitumi njia nyingine? kwa mfano anaweza kucheka na huko kunaweza pia kusababisha mapafu yake yakapanuka siyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…