OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Sina hakika kama ni Afrika nzima au Mtanzania tu.
Wengi wao akikupigia simu baada ya kupokea simu yake na akagundua kuwa haukuwa mlengwa, basi hukata simu ghafla bila maelezo yeyote.
Huwa kuna sababu gani ya kufanya hivyo? Je, ni uungwana? Mtu yule hata ukijaribu kumpigia ili kujua ana shida gani anaweza asipokee kabisa. Au akapokea lakini akajibu kimkato tu "Nimekosea nambaaaaa" kisha akakata
Je, hii ni hali ya kutojiamini kwa Mtanzania? Baada ya kugundua mpokeaji simu simu mlengwa, kwa nini usimweleze hilo kwa ufupi kisha mkaachana kwa amani badala ya kukimbia?
Miaka ya nyuma wakati mawasiliano ni gharama tungeweza kusema sababu ni kuokoa airtime maana "dola" zitaisha, mtu anaongea huku kidole kipo kwenye kitufe cha kukata. Lakini kipindi hiki ambapo madakika kibao, sioni haja ya kufanya hivyo.
Ni kumkosea heshima mtu anayekupokelea simu yako. Wengine tupo busy na tunajali namba ngeni, napoacha kazi zangu kwa ajili ya kukupokelea simu, halafu wewe unakata ghafla baada ya kusikia Haloo, nakuona hujiamini na pengine akili hazikutoshi