Hivi ni kwanini binadamu wengi wao, wakiwa hawana pesa huwa na ndoto za kila aina na zenye kuonyesha mtu huyu future yake ni sahihi na kubwa zaidi...!!
Lakini 'mfano' baada ya kuipata pesa ndoto zile hutoweka kwa kasi sana bila ya kutimizwa kama ilivyokuwa awali akifikiria?
Naombeni mnisaidie wanafamilia
#i'm fantastic boy
Tafuta maarifa ya kupanga,
kupanga siyo tu kuwaza nitauza magari, nitauza kompyuta, nitalima nyanya, nitafuga kuku.
ukiwa na mpango uliokamilika, ukipata hela unatekeleza lakini usipokuwa na mpango uliokamilika ndipo ukipata hela kila unachojaribu kushika unaona hakishikiki.
kama ni mpango wa kufuga kuku,
jiulize unataka kufuga ili iweje, labda ujasiliamali, sasa jiulize unalenga kupata pesa kiasi gani kwa mda gani? labda unataka laki 5 kwa mwezi, jiulize soko la kuku utalipata wapi? hapa anza kuuliza masoko ya kuku na utagundua ni kuku wa aina gani ufuge. Jiulize kwa aina hiyo uliyochagua je ufuge kuku wangapi ili kupata faida ya laki 5?
hapa utafanya mahesabu kulingana na ulivyoambiwa sokoni bei na gharama za kufuga.
hapo utajiuliza je unahitaji mtaji kiasi gani kufanya huo mradi, utapiga gharama za banda, kununua kuku wenyewe, matunzo kama chakula na madawa na mengineyo.
hapo utajiuliza je unaweza kupata pesa hiyo na kwa njia gani?
huo ndo mpango wa kufuga kuku unajua kila kitu.
sasa ukiwa na kitu kama hicho alafu ukapata pesa hiyo na usifanye basi utakuwa na matatizo.
ila kwa wengi kitu tunachokiita mipango siyo mipango na ndiyo maana tukipata pesa tunakosa cha kufanya.
tunachokiita mipango ni kusema nitafuga kuku nasikia kuku wanalipa, hujui gharama, hujui masoko, hujui mahitaji na sasa unapopata pesa ndipo unaanza kufanya mchanganuo na kugundua pesa uliyo nayo ama haitoshi au unaogopa changamoto.
KAJIFUNZE JINSI YA KUPANGA NDIPO UKIPATA PESA UTAPATA CHA KUFANYA