Hilo la laana umetudanganya, hakuna kitu kama kumtamkia mtu kitu alafu kikatokea, hua ni coincidence tu. Ingekua kweli leo hii ningekua sina hata shilingi kumi maana nimetamkiwa mabaya mengi mno.
Tukirudi kwenye kuumba, nadhani unaongelea kuumba kiumbe kama binadamu au mnyama, inabidi uweke mawazo ya ushirikina pembeni, huwezi tamka tu kitu kikatengenezeka, sound waves ni waves tu zinacause vibrations kwenye air molecules, hazina uwezo wa kujitransform na kutengeneza madini yakaunganika kua kiumbe, wanasayansi bado wanajaribu kutengeneza kiungo kimoja kimoja, mfano kuna artificial heart, skin e.t.c ni vitu complex sana maana ili utengeneze kitu inabidi ujue vizuri kinavyofanya kazi, bado vitu vingi hatuvielewi kiundani lakini tunajaribu kuvielewa, ipo siku uwezo utakuwepo wa kumanufacture karibia kila kiungo cha mwili, ukivunjika mguu tutakua tunakupachina mwingine na unapiga kazi vizuri tu. Tunahitaji karne nyingine ya development kufikia level hiyo.