Kwanini mwanga wa radi unawahi kuliko sauti

Kwanini mwanga wa radi unawahi kuliko sauti

Mzawa_G

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
669
Reaction score
1,475
Nadhani wengi wetu tumekuwa tukiwa na maswali ni kwanini wakati radi linapiga sauti huwa inawahi sana kuliko mwanga kufika huki ardhini au katika uso wa dunia

Sababu kubwa inayosababisha hivyo ni kwa kuwa mwanga husafiri kwa kasi sana kuliko kasi ya sauti japo kuwa mchakato wa kitendo hicho cha radi hufanyika katika eneo moja katika mawingu huko angani kwenye matabaka ya anga hewa.

Sauti husafiri kwa kasi ya kilomita 1,225 kwa saa huku mwanga ukisafiri kwa ya kilomita 300,000 kwa sekunde hapo unaweza kuona ni kwa vipi mwanga unavyokuwa na kasi kubwa sana wakati wa kusafiri kwake.

Radi huzaliwa mara baada ya msuguano wa mawingu huko angani katika mawingu ya mvua kadri msuguano unavyozidi kuwa mkubwa ndipo mawingu yenye + na yale yenye - huja pamoja na kuzalisha muwako mkubwa wa mwanga au ambao huelekea moja kwa moja chini ardhini.

Ule mwanga mkali uliozaliwa mara baada ya mawingu ya negative na positive kusuguana , wakati wa kupita kwake kuelekea chini ardhini huchana anga hewa ambapo husababisha sauti kubwa sana ambayo ndio huwa muungurumo wa radi tunaousikia huku duniani.

#🇬 🇪 🇷 🇦 🇱 🇩 

FB_IMG_1664548719984.jpg
 
Back
Top Bottom