Kwanini Mwenyezi Mungu ameniumba na hii Roho?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Sijui ni kwanini nimekuwa ni ' Mtu ' mwenye Huruma sana na ' Mtu ' mwenye Kusahau yale ' mabaya ' yote niliyotendewa na Watu mbalimbali. Na kuna ' Mtu ' mmoja pia aliwahi kuniambia ya kwamba Wema wangu ( Roho yangu nzuri Kiubinadamu ) ndiyo inanimaliza na kuniponza mara kwa mara hivyo nianze kufanya ' Mazoezi ' ya kuwa ' Mtu ' mwenye Roho mbaya na Katili kabisa kwani ndiyo nitafanikiwa zaidi na haraka.

Je ni kwanini Mwenyezi Mungu aliniiumba na hii Roho? Je hawezi kubadili gia angani ili kuanzia sasa na Mimi nikawa na Roho ya Kishalubela / Kikatili ili nianze kwenda sawa na Wale wote ambao huwa wananikosea? Na je Mwenyezi Mungu amekubali Mimi kuwa na hii Roho nzuri na ya Utu kwa Wanadamu Wenzangu ambao Wao malipo yao Kwangu huwa ni ya Kikatili na ya Kunitenda?

Kama kuna Mtu anajua dawa ya kunibadili niwe na Roho mbaya na ya Kikatili kuanzia sasa naomba aniambia nikainunue.

Nawasilisha.
 
MKUU SIKU ZOTE ROHO YA KUSAMEHE NI HAZINA YA MAISHA YA FURAHA KWA MHUSIKA
 
Ukitaka kufanikiwa, kuwa na roho ngumu kidogo.

You can’t be everybody’s benefactor and expect to make it or fully achieve whatever goals you’ve set for yourself.

Kuhusu mungu, hiyo ni imani tu. Si uhalisia.

Na imani na uhalisia ni vitu viwili tofauti kabisa.

Happy hump day.

Deuces.
 
MKUU SIKU ZOTE ROHO YA KUSAMEHE NI HAZINA YA MAISHA YA FURAHA KWA MHUSIKA

Yaani sijui inakuwaje unakuta Mtu huyo huyo amekukwaza tena vibaya kabisa lakini pale akiwa na shida au hitaji fulani akikushirikisha tu hapo hapo Moyo wa Huruma unakuingia, unasahau aliyokufanyia na kuwa nae bega kwa bega Kushirikiana nae. Kwanini Binadamu wengine hawana hii Roho? Mwenyezi Mungu ana ' Makusudi ' gani labda kwa Watu wenye Roho kama yangu ya Huruma na Utu?
 
Msiifanye mioyo yenu kuwa migumu.katika siku za kujaribiwa.gentacymine wewe Ni dawa lakini Kuna ugonjwa unakusumbua.mnaumwa
 
Uliona wapi dereva wa daladala akijipigia debe yeye mwenyewe?

Mpiga lelemama halichezi.
 

Mkuu endelea hivyo hivyo na uzidishiwe zaidi katika kipimo cha kujaa na kusukwasukwa.

*Genta Fanya kunitumia vocha ya Halotel ya li-ten yaani 10k ndani ya pm...niko majalala tena choka mbaya broo..

usiniangushe MTU wangu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…