Kwanini mwezi wa Ramadhani vyakula vinapanda sana bei wakati walaji wa mchana wanapungua?

Kwanini mwezi wa Ramadhani vyakula vinapanda sana bei wakati walaji wa mchana wanapungua?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nimewasikia baadhi ya viongozi wa Bakwata mkoani Shinyanga kupitia ITV wakilalamika kupotea kwa sukari na mfumuko wa bei za vyakula wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Viongozi hao wanadai wafanyabiashara wasio waaminifu wameficha sukari ili waje waiuze kwa bei ya juu pindi mfungo utakapofika siku chache zijazo.

Najiuliza tu kwanini vyakula vipande bei wakati wa mfungo ikitiliwa maanani walaji wa mchana wanakuwa wamepungua sana?

Maendeleo hayana vyama!
 
Mimi kinachonishangaza zaidi huwa ni sukari. Kila mwezi wa Ramadhani lazima sukari iadimike au ipande bei. Sijui kuna uhusiano gani kati ya bei ya sukari na mwezi wa ramadhani
 
Mimi kinachonishangaza zaidi huwa ni sukari. Kila mwezi wa Ramadhani lazima sukari iadimime au ipande bei. Sijui kuna uhusiano gani kati ya bei ya sukari na mwezi wa ramadhani
Tumsubiri FaizaFox anaweza kutupa darasa!
 
Mimi kinachonishangaza zaidi huwa ni sukari. Kila mwezi wa Ramadhani lazima sukari iadimime au ipande bei. Sijui kuna uhusiano gani kati ya bei ya sukari na mwezi wa ramadhani
Baada ya mfungo mwili huhitaji sukari ili upate nguvu. Vyakula vingi vya futari huwekwa sukari kama uji, chai, tambi nk.

Sukari hutumika sana mwezi wa Ramadhani.
 
Alieanzisha uzi kaandika vizuri sana ila kuna bata zitakuja kufanya ni uwanja wa dini na kejeli
 
Baadhi ya aina ya vyakula ikiwemo sukari lazima bei ipande hata wakati mwingine viadimike masokoni kwa sababu aina hizo za vyakula ni vinatumiwa sana na waislam kwenye kipindi hiki cha ramadhani
 
Huu Uzi umeuliza vizuri kabisa Ila baadae watauswitch utakuwa Uzi wa kidini sio sukari Tena ngoja waje wakulugwa!!
 
Sio vyakula vyote mkuu, ni vile ambavyo vinatumika sanaa kwaajili ya iftar, sukari inatumika sanaa mwezi wa ramadhan kuanzia chai, uji mpaka aina nyingine za iftar huwekwa sukari mfano, maharage, vipopoo , mihogo(sio wote huweka) n.k
 
Huu mwezi ndugu zetu huwa wanausubir kwa hamu kweli yani ni mwezi wa kulaa. Zile habari za kula Ugali dagaa hakuna tena. Kila siku ni kama sherehe. Ndyo maana hata mfungo ukiisha wengi huuumia sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kinachonishangaza zaidi huwa ni sukari. Kila mwezi wa Ramadhani lazima sukari iadimike au ipande bei. Sijui kuna uhusiano gani kati ya bei ya sukari na mwezi wa ramadhani
Unashangaa nini wakati post namba moja ina jibu tayari. Isome vizuri.
 
Mwezi wa Ramadhan ni mtukufu. Waislam hununua kwa wingi vyakula vyote muhimu ili kuvitawanya kwa familia zingine kama sadaka yao.

Obviously demand inakuwa kubwa kuliko upatikanaji ni lazima bei zipande.
 
Back
Top Bottom