OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Tusaidieni kujua, inaonyesha aliuawa 71 na kuzikwa 79.
#RIP ZHP
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aliuliwa na majeshi ya uvamizi wa Uganda,ilikuwa 1978,1979 vita iliisha,akazikwa kwa heshima zote
miaka 8 mwili ulikuwa wapi?Mwili ulikuwa Uganda tokea alipouawa 1971
Baada ya Vita mwili huo ulirejeshwa na ulizikwa kwa heshima zote alizostahili
Nafikiria Father and son relationship ( Zakaria Hans Pope na Hans Pope )Mkuu mbona kama unakimbia kuandika uzi.
Emvu weka wazi kwanza.. huyu Hans Pope na Huyu wa sasa wana uhusiano gani?
Copy and Paste..
nice👏Copy and Paste..
Kinda interesting!
leo nimeona nilete kidogo stori ya Baba yake Zakalia ambaye aliitwa Hans pope.
Huyu mzee alikuwa RPC wa west lake (mkoa wa ziwa maghalibi) mkoa huu ulihusisha Kagera ambapo alikuwa akifanyia kazi, wanajeshi wa Idd Amin walivamia sehemu ya Tanzania mwaka 1971 sio kwa nia ya vita bali kwa nia ya kuwaokoa wenzao ambao walijikuta wamezurula hadi sehemu ya Tanzania hivo wakaishia kutekwa na askari wa Tanzania
Kuna story nyingi juu ya sababu ya wanajeshi hao wa Uganda kuingia Tanzania,lakini ya kuaminika ni kwamba walifika eneo la Tanzania kufuata maji na hivo wakatekwa,wenzao walipopata taarifa waliona hawawezi ku report makao makuu ya jeshi la Uganda hili suala bali wakaamua kuja kuwaokoa wenzao.
Wanajeshi wa Uganda ambao walikuwa ni wachache walifanya ujinga wa kuja na vifaru viwili na badala ya kuokoa wenzao walimkuta Hans pope (RPC) akiwa na dereva wake kwenye land rover wakaamua kumfuata, RPC alivoona anafuatwa na wanajeshi wa Uganda akaanza kukimbia akapige radio call kutaarifu makao makuu uvamizi wa wanajeshi wa Uganda, lakini kabla hajafikia Radio Call alipigwa risasi kwenye paja na akaanguka chini, dereva wake naye alivoona hivo alishuka na kuanza kukimbilia Radio call lakini naye alipigwa risasi ya mguu na kuanguka,akiwa chini huyo dereva alijaribu kushika bunduki ndipo akapigwa risasi nyingine mkononi na wanajeshi wa Uganda ambao walifika na kumchukua RPC pope
Kwa mujibu wa mashuhuda RPC aliwasihi wanajeshi wa Uganda wasimuue lakini wakambeba na kwenda naye Uganda ambapo Idd Amin alitangaza kwamba Hans Pope ni mamluki wa kichina aliyevamia Uganda (hapa Idd Amin alidanganywa na wasaidizi wake), basi Hans pope aliteswa na kuuawa na baadaye aliwekwa mwili wake maonesho kwa siku tatu (uliwekwa dawa usiharibike).
Baada ya hapo, wanajeshi wa Amin waliupeleka mwili wa Hans pope huko hospitali ya Mulago na kuwapa madaktari kisha wakaondoka bila kutoa maelekezo. Madaktari waliamua kwa siri kubwa kuchukua jukumu la hatari la kuuwekea kemikali za kuutunza kwa miaka 30. Lakini ilikuwa kazi ngumu kwa sababu marehemu Hans pope alidungwa visu karibu kila sehemu ya mwili na alikuwa na majeraha ya risasi hivo basi dawa za kutunza mwili alizochomwa zilitokea kwenye mashimo ya vidonda.
Baada ya miaka 8, idd amin alitolewa madarakani na mwili huo ulikabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania ambapo ulizikwa huko Iringa.
NB
Zakaria na kaka yake walienda vitani kumuondoa Idd Amin nchini Uganda na wakati huo Zakaria alikuwa ni captain wa JWTZ
Kuna watu wavivu sana kusoma au kupekua. Hii stori ilishaandikwa muda mrefu hapa JF. Lakini pamoja na kuwa imeletwa tena, haitashangaza kukutana na maswali ambayo majibu yake yameshaandikwa hapa!Copy and Paste..

Mtu na mwanawe, huyu wa sasa ni Zakariah Hans pope,Mkuu mbona kama unakimbia kuandika uzi.
Emvu weka wazi kwanza.. huyu Hans Pope na Huyu wa sasa wana uhusiano gani?
Baba yakeMkuu mbona kama unakimbia kuandika uzi.
Emvu weka wazi kwanza.. huyu Hans Pope na Huyu wa sasa wana uhusiano gani?
Okay okayNafikiria Father and son relationship ( Zakaria Hans Pope na Hans Pope )
Okay okay.. notedMtu na mwanawe, huyu wa sasa ni Zakariah Hans pope,
OkayBaba yake
miaka 8 mwili ulikuwa wapi?
Baada ya Idi Amini kumpindua Rais Milton Obote na kuingia madarakani nchini Uganda mwaka 1971 alianzisha vitimbi dhidi ya Tanzania vilivyopelekea misuguano ya kijeshi ya mara kwa mara mpakani Mtukula/Misenyi nk. RPC wa Mkoa wa Ziwa magharibi sasa Kagera SACP Hans Poppe alijikuta yeye akiwa mstari wa mbele kutuliza ghasia hizo kipindi hicho mkoani Kagera hakuna kikosi cha jeshi JWTZ kama ilivyosasa Kaboya; katika moja ya tafurani kama hizo mpakani SACP Hans Poppe ndipo alipigwa risasi akauawa majeshi ya Uganda yakawahi mwili wake yakichukua kwenda kusambaza propaganda kwamba Tanzania ilikuwa unasaidiwa na majeshi ya kigeni hususani wachina kuishambulia Uganda! Wakauchukua mwili wa Hans Poppe na kuufanyia matangazo mengi kwenye Televisheni na Magazeti kushamirisha propaganda yao, licha ya jitihada zote za kijasusi kijeshi na kidiplomasia Idi Amini alikataa katakata kuuachia mwili wa SACP Hans Poppe! Ilikuwa ni baada ya vita vya Oktoba 1978 mpaka aprili 1979 kati ya Uganda na Tanzania, majeshi yetu yalipouteka mji wa Kampala na kumfurusha Idi Amin ndio majeshi yetu yaliweza kuupata mwili wa RPC Hans Poppe na kufanya utaratibu wa kuurudisha nyumbani, nafikiri Kapteni Zakaria Hans Poppe, naye sasa marehemu ndiye aliyekabidhiwa mwili huo kwa niaba ya familia na hatimaye ukasafirishwa hadi nyumbani kwake kwa mazishi rasmi mwaka 1979.