Kwanini "mwonekano" ni kigezo muhimu kwa msanii?

Kwanini "mwonekano" ni kigezo muhimu kwa msanii?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Wanaita 'star look' right? YES!

”Leo kwenye ustaa simo kisa sina mwonekano!” ~Msodoki.

Sikuwahi kuwaza hili, japo hisia tu na kuona kila 'msanii' anahangaikia mwonekano fulani. Iwe ni msanii wa kuimba au filamu, ukiacha sanaa za asili na wale wacheshi ambao nao wanajua wenyewe.

Sasa nikaisikia kupitia Bongo Star Search, BSS. Kwamba sio tu uwezo wa sauti na kuimba, bali unahitaji kuwa na 'a star look' ili uuzike!

Hii maana yake nini, mbona tunaona wasanii wengi tu wenye mionekano ya kawaida! Au ndo sababu ya kuvaa miwani na mavazi ya ajabu ajabu?

Swali la msingi:

Mwonekano unahusiana vipi na kazi ya sanaa?
 
Huo ujinga wameu invert wasafi hapa nchini?
Kwani gurumo alikuwa alikuwa na mwonekano gani? Mbona na alikuwa anaimba vizuri
 
Tatizo ubunifu hakuna,mtu akiona mwenzie katrend kwa style flani basi na yeye anaiga
 
Hata kwenye filamu, mimi Kashaulo sijawahi kuigiza kama boss maisha bora ofisi kuuubwa!

Kinyambe aliishia kuwa mcheshi na mfungua mageti tu.
 
Suala la muonekano halipo kwa wasanii peke yake,hata watu wengine muonekano ni kitu muhimu sana, muonekano wako, uvaaji wako, uongeaji wako nk vinatoa tafsiri nyingi sana kuhusu wewe.

Inapowezekana tujitahidi tuwe kwenye hali nzuri a muonekano kwa kadri ya uwezo tulionao.
 
Back
Top Bottom