Kwanini mzazi analazimika kumlipia Tsh 400,000 mwanaye anayesoma shule ya Serikali ya Kiingereza wakati Serikali inatoa elimu bila malipo?

Kwanini mzazi analazimika kumlipia Tsh 400,000 mwanaye anayesoma shule ya Serikali ya Kiingereza wakati Serikali inatoa elimu bila malipo?

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
5,200
Reaction score
12,762
Waziri wa Elimu, Prof. Adolph Mkenda naomba utusaidie maelezo ya kina kuhusu shule za msingi za serikali zinazofundisha kwa lugha ya kiingereza.

Swali ni moja tu, KWA NINI MWANACHI ANALAZIMIKA KULIPA SHILINGI 400,000+ YA ADA KWENYE SHULE HIZI wakati ambao serikali inatekeleza sera ya elimu bila malipo ya ada?🤔

Kwa nini mwananchi analazimika kulipa ada zaidi ya laki nne kwenye shule ya umma, iliyojengwa kwa fedha za umma, kwa malengo ya kutoa elimu bure kwa umma?

Mwalimu anayefundisha kwenye hizi shule ni wa serikali, mshahara analipwa na serikali, vitabu vinanunuliwa na serikali, na mengine yote. Hiki kinacholipiwa ni kitu gani?

Tofauti iliyopo kati ya shule hizi za umma ni lugha ya kufundishia tu. Kwamba wakati shule nyingine zinatumia kiswahili kama lugha ya kufundishia, hizi zinatumia kiingereza kama lugha ya kufundishia.

Kwa nini tofauti ya lugha tu imfanye mwananchi kulipa ada kwenye shule ya umma? Je, shule hizi zitakuwa na huduma tofauti na shule za Kiswahili? Kama ndio, kwa nini kuwe na utofauti?🤔

Yani, kwa nini mwananchi ambaye mtoto wake anasoma shule ya umma ya Kiswahili asilipe ada lakini mwananchi anayepeleka mtoto kwenye shule hiyo hiyo ya umma lakini inayotumia lugha ya kiingereza alipishwe ada, tena zaidi ya 400,000?🤔

Lakini pia wote tunaelewa kuwa elimu ni huduma, SIO BIASHARA (katika tafsiri ya serikali), na kwamba kila raia wa Tanzania ana haki ya kupata elimu hiyo by merits pasipo kubaguliwa.

Hata hivyo tunaelewa pia kwa mujibu wa takwimu zetu, zaidi ya 1/3 ya watu wazima Tanzania, yani watanzania zaidi milioni 20, wana kipato kisichozidi elfu 49 kwa mwezi.

Je, watoto wa watanzania hawa watawezaje kusoma kwenye shule za umma za kiingereza ikiwa mmeweka geti kubwa la malipo? Ipo wapi haki ya watanzania hawa kusoma kwenye shule za umma na kupata elimu pasipo kubaguliwa?🤔

Lakini pia natamani kujua, ni nini logic ya serikali kuanzisha shule za umma za kulipia zinazotumia lugha ya kiingereza kama lugha ya kufundishia huku shule nyingine zote zikitumia Kiswahili kisha baadae kuwalazimisha wanafunzi wote kusoma kwa kiingereza wanapofika sekondari?

Hawa ambao hawakuandaliwa kwa lugha ya kiingereza kwa sababu ya kusoma kwenye shule za umma za Kiswahili na kushindwa kulipia shule za umma na binafsi za kiingereza mna mpango gani nao?

Wao sio watanzania?

Wao hawastahili kupata elimu na maarifa kwa lugha wanayoielewa?

Kama kweli kiingereza mnachofundisha shule za msingi za umma kinatosha kumwandaa mtoto kusoma kwa kiingereza sekondari, hizi shule za kiingereza mnazoanzisha ni za kazi gani?🤔🤔🤔

Naomba pia kuwauliza wadau wa taasisi ya haki za binadamu je hili jambo ni sawa?

Chanzo: Onesmo Mushi (Ukurasa wa x)
 
Naaaam, kwa kuongeza tu, kwa nini hizi shule zisiwe nyingi? Maana inaonekana demand ni kubwa kuliko upatikanaji wa nafasi
Kama taifa tunapaswa kuwa na msimamo ni lugha ipi iwe inatumika shuleni,sio hivi ilivyo sasa na ukweli wazazi wengi wangekuwa na uwezo wangewapeleka watoto wao kwenye hizo za kutumia kiingereza.
 
Waziri wa Elimu, Prof. Adolph Mkenda naomba utusaidie maelezo ya kina kuhusu shule za msingi za serikali zinazofundisha kwa lugha ya kiingereza.

Swali ni moja tu, KWA NINI MWANACHI ANALAZIMIKA KULIPA SHILINGI 400,000+ YA ADA KWENYE SHULE HIZI wakati ambao serikali inatekeleza sera ya elimu bila malipo ya ada?[emoji848]

Kwa nini mwananchi analazimika kulipa ada zaidi ya laki nne kwenye shule ya umma, iliyojengwa kwa fedha za umma, kwa malengo ya kutoa elimu bure kwa umma?

Mwalimu anayefundisha kwenye hizi shule ni wa serikali, mshahara analipwa na serikali, vitabu vinanunuliwa na serikali, na mengine yote. Hiki kinacholipiwa ni kitu gani?

Tofauti iliyopo kati ya shule hizi za umma ni lugha ya kufundishia tu. Kwamba wakati shule nyingine zinatumia kiswahili kama lugha ya kufundishia, hizi zinatumia kiingereza kama lugha ya kufundishia.

Kwa nini tofauti ya lugha tu imfanye mwananchi kulipa ada kwenye shule ya umma? Je, shule hizi zitakuwa na huduma tofauti na shule za Kiswahili? Kama ndio, kwa nini kuwe na utofauti?[emoji848]

Yani, kwa nini mwananchi ambaye mtoto wake anasoma shule ya umma ya Kiswahili asilipe ada lakini mwananchi anayepeleka mtoto kwenye shule hiyo hiyo ya umma lakini inayotumia lugha ya kiingereza alipishwe ada, tena zaidi ya 400,000?[emoji848]

Lakini pia wote tunaelewa kuwa elimu ni huduma, SIO BIASHARA (katika tafsiri ya serikali), na kwamba kila raia wa Tanzania ana haki ya kupata elimu hiyo by merits pasipo kubaguliwa.

Hata hivyo tunaelewa pia kwa mujibu wa takwimu zetu, zaidi ya 1/3 ya watu wazima Tanzania, yani watanzania zaidi milioni 20, wana kipato kisichozidi elfu 49 kwa mwezi.

Je, watoto wa watanzania hawa watawezaje kusoma kwenye shule za umma za kiingereza ikiwa mmeweka geti kubwa la malipo? Ipo wapi haki ya watanzania hawa kusoma kwenye shule za umma na kupata elimu pasipo kubaguliwa?[emoji848]

Lakini pia natamani kujua, ni nini logic ya serikali kuanzisha shule za umma za kulipia zinazotumia lugha ya kiingereza kama lugha ya kufundishia huku shule nyingine zote zikitumia Kiswahili kisha baadae kuwalazimisha wanafunzi wote kusoma kwa kiingereza wanapofika sekondari?

Hawa ambao hawakuandaliwa kwa lugha ya kiingereza kwa sababu ya kusoma kwenye shule za umma za Kiswahili na kushindwa kulipia shule za umma na binafsi za kiingereza mna mpango gani nao?

Wao sio watanzania?

Wao hawastahili kupata elimu na maarifa kwa lugha wanayoielewa?

Kama kweli kiingereza mnachofundisha shule za msingi za umma kinatosha kumwandaa mtoto kusoma kwa kiingereza sekondari, hizi shule za kiingereza mnazoanzisha ni za kazi gani?[emoji848][emoji848][emoji848]

Naomba pia kuwauliza wadau wa taasisi ya haki za binadamu je hili jambo ni sawa?

Chanzo: Onesmo Mushi (Ukurasa wa x)
Hapo unalipia lugha ya kingereza hiyo laki 4.

Inashangaza sana, lugha ikiwa kiswahili ni bure, ikiwa kingereza ni laki nne

Mkenda inabidi aamue tuu moja kuwa lugha ya kingereza itumike msingi hadi sekondari ili kuondoa hayo matabaka
 
Kiingereza ni balaa
Kuna shule hapo Ubungo kuna tetesi inavunjwa ili iwe English medium la sivyo ina maana ingebaki kuwa hivyo hivyo ilivyo 😄
 
Back
Top Bottom