Kwanini nakuwa na mawazo ya hivi?

Kwanini nakuwa na mawazo ya hivi?

Joined
Sep 10, 2019
Posts
17
Reaction score
15
Ndugu zangu naomba msaada wa kimawazo,

Kama mwezi mmoja hivi kunawakati nilikuwa mtu mchovu mchovu, kuamka mapema yenyewe ilikuwa shida, nikawaza labda nijaribu kuwa nafanya mazoezi ,lakini changamoto ikawa mazoezi yenyewe nikawa sifanyi kama nitakavyo nasema kesho kesho na ikitokea nimefanya basi nafanya mara moja labda jogging tena nikiwa na company au kuruka kamba.

Sasa hii hali ikatengeneza maswali mengi kwenye akili yangu kuhusu mazoezi yaan watu husema mazoezi Ni muhimu ,"

Je, inamaana siku zote za maisha yangu nitakuwa nikifanya mazoezi, na kipindi nikiacha itakuwaje na Kama mazoezi Ni muhimu kwa afya mbona baadhi ya watu wengi hawafanyi mazoezi na wapo vizuri kama wazazi wangu,

Mwingine hajawahi jihusisha kabisa na yupo pw nikiwa barabaran nikimuona mtu anajogg najiuliza inamaana huyu mtu hufanya kila siku na vp ikitokea hafanyi labda, ambapo haya mawazo nikiwa sina majibu nakuwa sina raha kabisa nakuwa depressed kabisa.
 
Zingatia lishe bora na penda sana kutembea kama safari si ya kuhitajia usafiri.
 
Mazoezi ni kipimo cha commitment.

So, hapo unaweza kuweka commitment nyingine halafu mazoezi yakawa for fun.
Mimi niligundua mazoezi ya jogging na kuruka kamba hayanifai yaani sipati motisha.

Nikaamua football nankwasababu ni mchezaji mstaafu hahaaaa nikarudia daruga mambo inogile...nfanya tizi, naenjoy, imake jokes, I interact huku mwili unapata stahiki yake.

Mkuu, life haitakiwi kuwa boring kama ulivyoandika hapo maana yake uko bored with alot of things in your life. Stop it. Mwishowe utaingia ktk pressure, mwili kukosa nguvu na depression.

Jichanganye. Nenda maskani, laugh moderately, speak with people, tafuta friends hata wawili different genders mbadilishane mawazo.
 
Back
Top Bottom