Pole sana kaka,
Kuna siri moja ipo katika ndoto ambayo watu wengi haitambui ama na hata kujua kama ipo,
Mara nyingi wale wanaofasiri ndoto huwa wanatafasiri kutokana na udhoefu wa ndoto husika au wahusika wa ndoto yenyewe haswa kulingana na asili pamoja na tabia za wahusika.
wahusika yaweza kuwa mtu,jiwe,miti,mnyama nk
Ukweli wa ndoto umekuwa ni kinyume kabisa ama ni tofauti kabisa na huwa hairilate kabisa wahusika na maana yake japo yaweza kuelekeana kidogo lakini si mara zote kama watafasili wanaotupa ndoto hufanana.
Usichoke haka kautangulizi kazuri sana huenda ukawa nawe mtaalamu wa ndoto pia.
Mwili ulivyoumbwa wenyewe asili yake una nguvu ya asili ambayo mara nyingi huwa inajiamsha yenyewe(activation) au mda mwingine hadi ichochewe kidogo.
Matokeo makubwa ya hii kitu huweza kuleta taarifa kwa njia ya ndoto (japo kitaalamu si kila utaota ni ndoto zingine ni mwitikio wa mwili tu)
mfano kuna mtu kila akiota ndoto gari imegonga mti ama imeanguka huwa wanapata msiba katika ukoo wao na ndoto zinazohusiana na hizo, lakini kumbe kitaalamu inakuwa hiyo ni respond ya ile natural power ya mtu kutokana na kwamba mwili unaweza ukahisia kitu ama kutambua pasipo akili yako kujua ama kabla hakijatokea na mara zote hizi huwa sio ndoto(Kitaalamu) bali ni matokeo ile nguvu ya asili ya mwanadamu.
Kuna tiba ya ushauri na baadhi ya mazoezi ya kufanya ile inner power isiwe inajiendesha yenyewe(watu wene elimu ya tai chi wanafanikiwa zaidi katika hili zoezi la kukontro inner power ambayo ndio hiyo nguvu ya asili)
Sasa ni nini ukweli wa tafasiri za ndoto?
Ndoto ina misingi ya ukweli miwili tu ya kutoa maana ni kupitia Mungu ama kupitia shetani.
Ndoto ni njia ambayo nafsi inafanya mawasiliano katika ulimwengu wa roho sasa lugha inayotumika katika ulimwengu huo si sawa na lugha ambayo tunaiweka katika masuala ya mazoea.
Na watu amabo wamesimama vizuri katika dini ndio huweza kujua kiurahisi maana za ndoto kutokana anakuwa upo karibu zaidi na mazingira ya ulimwengu wa rohoni.
mfano ukiangalia ndoto za watu wa kwenye vitabu vitakatifu na ukija kuangalia maana zake unakuta ni tofauti kabisa na jinsi ambavyo sisi huwa tunapeana maana na ndoto tunazoziota.
Nimeongea japo kiufupi tu kuhusu jambo hili la ndoto japo zipo elimu nyingi sana juu ya ndoto ambazo ukiamua kuzisoma ndio utatambua kila elimu mapungufu yake na ipi iko bora zaidi.
SASA NAINGIA KATIKA TAFSIRI YA NDOO YAKO.
Kuna mambo mahache ningeweza kukuuliza kuhusu hiyo ndoto ili nipae mazingira mengi ya uhalisia na nitoe jibu zuri na kamili maana ndoto umeisimulia kama utangulizi tu.
Ila maana yaweza kuwa hivi
Huyo mwanamke anasimamia alama ya uzalishaji ambapo ni jumla ya uzalishaji wako binafsi ambapo tukileta katika uhalisia inakuwa ni uchumi wako binafsi.
yaonyesha unamiradi ambayo unaendesha ama umeipanga kuiendesha pia ipo miradi ambayo umeijua lakini haujaimini kama ndio inaweza kukuzalishia na kukufikisha mahali ambapo unahitaji.
na pia yaonyesha hiyo ndio miradi ambayo inaweza kukunyanyua zaidi kiuchumi tofauti na ambavyo ungetarajia.
kwahiyo ni ndoto inayolenga kukueleza juu ya uchumi wako binafsi unavyoweza kupambana nao.
Ushauri:
1.Ongeza mawasiliano na watu hasa wafamilia yako hasa wale unaoishi mbali nao yaweza kuwa wapo kijijini kwenu au sehemu nyingine, pia hata kuwatembelea ndugu walio mbali nawe hasa kijijini kwenu.
2.JAribu kushirikisha marafiki zako mipango yako lakini iwe kwa kauli kama zakutaka kujua wao kw akili zao wangefanyaje japo si wote waweza kuwashirikisha.
Nyongeza:
Pia Yaweza Kuwa mafanikio yako yapo ulikotokea.
Hitimisho.
Ila Tafasiri yangu yaweza kwena tofauti na fikra zako Kumbuka MUngu ndiye atupangiae kila jambo Ibada Yako ndio Muhimu kwako