Kwanini naunga mkono tozo

Sasa hivyo vyote ulivyotaja sijui madini, gesi etc huko kote kunakatwa kodi, kuisikia madini maana yake wachimbaji wanachi ba then serikali inawakata kodi
 
Hakuna anaekataa serikali kuweka tozo hata mimi nalipa kwenye miamala ya simu na mkononi na kwenye akaunti benki.

Hii kodi kwanza ipitishwe na bunge baada ya kujadiliwa na kisha iwe "justified" yaani ielezwe wapi yaenda na itafanya nini.

Vinginevyo serikali ikijiamulia kuweka tu tozo inakuwa yawaonea wananchi.
 
Anasahau kilimo kina tozo kwenye mazao kama Korosho, Kahawa na mazao mengine. Ukisema ufugaji kuna tozo kwenye machinjio, ambako wanyama hupelekwa ili tupate nyama.

Hii ya ufugaji serikali yaweza kuweka sheria kwamba hakuna mtu kujichinjia tu mnyama mahali iwe kitimoto au ng'ombe au mbuzi ni lazima iwe machinjioni na kule itapata fedha za tozo ya machinjio.

Kwenye kilimo wafugaji wawekewe fedha benki yao na iwezeshwe kwelikweli ili wakope kisha wanunue pembejeo na vifaa vingine kama matreka na mashine zingine kubwa za kilimo na kipaumbele kiwe kwa wakulima wa kitanzania.

Hawa wakulima na wafugaji wakiwezeshwa ndani ya miaka 10 tunapata wakulima matajiri wenye mashamba makubwa na watazalisha mazao mengi na mifugo yao itatoa chakula na bidhaa zitauzwa kisasa.

Ndo maana ya kuwekeza kwenye kilimo na sio kuleta kauli za tunawekeza kwenye kilimo bila ufafanuzi wafanya vipi.
 
Tozo ni nzuri iwapo zitafanya kazi za maendeleo lakini sio kununua ma viete na kulipatana maposho mlima.

Uliiona ile nyumb ya mil. 13.5!?? Hayo ndo yatukera sasa.!
 
Ukisikia uzalendo ndio huu.
P
 
Sina ujuzi mzuri waku speculate kiuchumi. Ila nachojua tu ni zile taarifa za kuingia uchumi wa kati, huku miradi mikubwa ikianzishwa na kutekekezwa, huku tahadhari kubwa ikifanywa kuto kumuathiri mtu wa chini...
 
Kodi zitozwe kwa wenye vipato vikubwa, rushwa idhibitiwe, mali za waliopatikana na hatia zitaifishwe na kurudishwa serikalini.

Kumbuka hata huko kwenye uwekezaji wa kilimo hela zitapigwa huko huko...
 
Kuna msema maarufu usemao "no tax without representation". Watanzania hatuna wawakilishi tuliowachagua, bali walijichaguliwa na mfumo. Kama wawakilishi waliochaguliwa na watu wangelikuwa kwenye vyombo vya uwakilishi wasingepitisha kila kitu cha serikali bila kuangalia madhara yake. Unakumbuka waziri mwenye dhamana kujitokeza na kukiri eti kuna kasoro katika muswada wa tozo? Hao wanaojiita wawakilishi wa wananchi walikuwa wapi? Kwa kifupi usilinganishe mfumo wa TZ na US.
 
Mwigulu Lameck Nchemba mlamba sali akileta ujinga wa kusadikika wa kuishi Texas nchini Marekani. Kila limbukeni anahisi akitaja kwa babu Biden ndo ataonekana wa maana eti!. Wananchi wanataabika kwelikweli Mwigulu Madelu anatamba na v6 ya milioni ya Mia tano sitini (560) halafu tunadanganywa na solidarity Fund!. Huu mfuko wa MSHIKAMANO unaotuumiza wananchi kwa kiasi kikubwa na cha kutisha chanzo chake ni wapi na ulipitishwa na nani?. Huu ni mfuko wa kifisadi, kifedhuli na kizandiki wa Mwigulu na Musa Hassani Zungu!. Ni taabu na shida kuwa na wabunge wa ndiyo mzee katika nchi iliyo na zaidi ya miaka 60 tangu Uhuru.

Uchafuzi wa 2019 na 2020 ndo chanzo cha ufisadi, dhuluma na kila aina ya ukandamizaji unaoendelea katika nchi hii. Mtumishi anakatwa PAYE halafu Tena anapachikwa tozo Benki!.

Wewe mzee wa mawe uishi ukifahamu taabu ambayo mamilioni ya watanzania wanaipata wakati familia yako inaishi maisha ya kifahari na anasa ya viwango vya kutisha.

Enyi Mbowe Freeman,Tundu Lissu, John Mnyika na viongozi wengine wandamizi wa upinzani mmefanya makosa makubwa Sana ya kunyamazia dhuluma inayoendelea katika nchi hii kwa kigezo kuwa mmeishalamba asali. Tumebaki na upinzani maslahi na upinzani matumbo!. Enzi za Dr. Wilbroad Slaa uozo huu unaoendelea usingekuwepo. Yupo wapi Ruyagwa Zitto Kabwe?. Zitto analamba asali kule Zanzibar kumbe hawezi kukosoa tena dhuluma na ukandamizaji wa tozo unaoendelea katika utawala huu.


Pumzika kwa amani jabali la Tanzania na Africa Dr. John Pombe Joseph Magufuli ulifahamu maji yaliyokuwa yakichemka jikoni ukatuambia "tutakukumbuka". Tunakukumbuka na kukulia Sana baba Kwan leo kilo moja ya mchele wa 1200/ wkt wa uongozi wako leo hii ni 2500, mafuta Lita 20 kwa 57,000/= wakati wako leo hii ni laki 1 na elfu 20, kilo moja ya unga wa mahindi kwa sh 700/= leo ni 1800/=, kilo moja ya ngano kwa sh. 1200/= leo hii n 2000/=. Tunakukumbuka Sana baba na daima tukuenzi na kuziishi fikra zako.
 
Sasa hizi General assemblies zao wadiwani wa mchongo huketi na meya wa mchongo kufanya vikao ambavyo ni lazima bajeti ipite bila kupingwa na bila kuchunguzwa.

Kisha ikipitishwa madiwani wa michongo hulipoana poshi za michongo na kesi closed, huu ni ufisadi.

Madiwani wakiwa na meya ambae amechaguliwa na wananchi hawatafanya upuuzi huo kwani meya atakataa maana anawajibika moja kwa moja kwa wananchi na siku zote yupo tayari kutetea maslahi ya wananchi ndani ya eneo lake.
 
Kuna mambo mengi tu ambayo wanaweza kufanya ili kupata hiyo Trillion.

Wananchi wangeliwaelewa kama walau wangepunguza matumizi yao binafsi kama vile kuacha kununua mgari mengi ya kifahari kama maV8. Pia wabunge na wafanyakazi wote wa serikali wangeondolewa sitting allowance. Haiingii akili mtu analipwa sitting allowance kwa kufanya kazi yake ...... Na mwisho kabisa Wabunge wakubali kulipa kodi kwa kipato chao i.e. mishahara na malupulupu yao.

Kama wakifanya hivyo na hiyo Trillion haitimii ndiyo warudi kwa wananchi kujazia......!!
 
Huu uzi akiuona nchemba tumeumia, maana jamaa kamtajia maeneo mengine ya kuweka tozo, daah
 
1. Haya yote uliyoandika tunayajua vizuri pengine kuliko wewe ujuavyo...

2. Kwa kifupi sana ni kuwa, wewe hujajua ni nini kinacholalamikiwa na wananchi wa Tanzania...

3. Laiti ungejua, likely ungekuwa na maoni tofauti na hiki ulichoandika hapa...

In short;

✓ Watanzania tunajua umuhimu wa kulipa kodi...

✓ Watanzania hatulalamiki TOZO ili tusilipe kodi kwa jina lolote lile kama ambavyo umejaribu kushawishi akili ndogo...

Kinacholalamikiwa kuhusu TOZO hizi mpya na kupigiwa kelele sana na wananchi kiasi cha watu kwenda mahakamani ni haya na ni vyema ukatoa maoni yako kwa kujikita katika hayo:

1. Kodi/tozo au sema jina lolote inatozwa kwenye pato gani..?

2. Huko ktk nchi uliko wananchi mnatozwa kodi mara mbili hata mara tatu au nne ktk pato la pesa ileile wakati uleule (double taxation?)

##Hebu jibu hili haraka labda tutakuelewa..

Labda utasema hujaelewa. Ngoja nikupe mfano wa mfanyakazi wa mshahara wa Tanzania uone anavyolimwa kodi nyingi kwa wakati mmoja kwa mshahara uleule..

##Mfanyakazi X ana mshahara wa TZS 1,000,000 kwa mwezi. Huyu sikiliza kodi anazokatwa na serikali hiyo hiyo moja..

Analipa;

•PAYE kila mwezi 270,000

• Akilipwa mshahara huo kupitia benki serikali hiyo hiyo inauguata huko huko benki kwa ajili ya kodi nyingine iliyopewa jina la TOZO kwa kila kiwango cha pesa anachotoa toka benki...

• Wakati huohuo benki inamtoza charge mbalimbali za kumtunzia pesa huyu mfanyakazi X toka mshahara huohuo wa fedha yake ambazo serikali inachukua kodi toka kwake mtoa huduma yaani (benki)...

✓ Hicho ndicho kinacholalamikiwa ndugu. Watu si kwamba hawataki au hawapendi kulipa kodi. Tunapenda sana na tunajua umuhimu wake. Lakini tumeshachanganywa na waziri Mwingulu Nchemba kiasi cha kujiuliza anatumia mfumo gani ku - introduce kodi.

Kwani badala ya kuwafanya wapende na wajitoe kulipa kodi, badala yake anakaribisha malalamiko na manung'uniko kwa sababu tunaamini serikali sasa inatumia kisingizio cha kodi kupora/kuibia watu pesa zao kwa nguvu...!!

Hebu tujadili katika mwelekeo huu na sivyo unavyoelewa wewe...
 
Nchi zenye uwazi na uwajibikaji 0 unafananisha na nchi zilizoendelea mkuu?

Kwa sasa hakuna bidhaa/huduma ambayo haijapanda bei walau kwa kudouble price ya bei ya zamani kwa bidhaa husika, serikali imefanya nini kuhusu hilo? Hata kulizungumzia hawajawahi. Lakini huyo huyo mwananchi kwa kipato kile kile anaongezewa na tozo hapo hapo.

Tuliambiwa Mikopo kadhaa ikiwemo wa Covid na mwingine kutoka IMF umepelekwa kwenye madarasa, vituo vya afya, barabara vijijini, Hapo hapo tunaambiwa tozo zinapelekwa katika projects hizo hizo, Basi zimekusanywa shilingi ngapi, zikapelekwa wapi na hivyo vitu vilivyofanyika viko wapi? Haijulikani zaidi ya maneno matupu. Katika mazingira kama haya huyu mlipa kodi/tozo aendelee kuwa na imani na wakusanya kodi/tozo? Na je aendelee kuunga mkono?

Kwa taarifa tu kama mtu anatembea Tz huko kwenye wilaya zake, atakubaliana na mimi kwamba kuna madarasa yalijengwa kipindi cha Rais Magu Binafsi niliyaona kusini Mbinga& Nyasa tangu mwaka 2020. Lakini chakusangaza Leo hii yanaitwa madarasa ya pesa za Covid! 2020 Covid???
 
Unawezaje kufananisha kipato cha mtu wa Texas na mtu wa Buza kwa Mpalange?
 



Huko ktk nchi uliko wananchi mnatozwa kodi mara mbili hata mara tatu au nne ktk pato la pesa ileile wakati uleule (double taxation?)

Hivyo malalamiko ni kwa wafanyakazi wa serikalini pekee?. Makato ya mfanyakazi sita ongelea au kulinganisha na nchi nyingine.

Double taxation zipo ingawa watu hawajui mfano kampuni zinalipa kodi na wamiliki wa kapuni ambao ni shareholders wanalipa kodi tena kutokana na kipato kilekile.

Kwa ujumla wake Watanzania ni walalamishi wakati huohuo hawafuatilii mambo wakati yakitokea. Bunge limekaa na kujadili hili mlikuwa hamsemi lolote, serikali wakati inatoa mapendekezo wazi kwa umma mlikuwa hamsemi chochote kwasababu mlifikiri ni wengine ndiyo watalipa. Imefika wakati badala ya kulalamika tafuta kipato zaidi. Tanzania ni nchi ambayo uzalishaji ni mdogo sana kiasi kwamba vitu kama hivi vitalazimisha watu wafunguke na kwenda kujishughulisha na uzalishaji. Wananchi wanatakiwa wahoji baada ya mwaka hiyo miradi ya umwagiliaji lakini vilevile tuhoji wale ambao hawajishughulishi. Lakini wafanyakazi wa serikali wasilalamike kama kazi za serikali hazilipi kajiendeleze kwa kutafuta sehemu nyingine. Karibu Dunia nzima kazi za serikali nyingi ni za viwango vya chini. Tumia muda mwingi hapa kutafuta namna nyingine za kipato na kuuliza maana utakuwa una lalamika kila mwaka huu ndiyo mfumo mpya wa nchi. Tozo zitapungua pale tu uzalishaji ukiongezeka. Badala ya kulalama husle ndugu yangu hao wengine ni watanzania kama wewe.
 

Akili za kulinganisha bei ya litre ya fuel USA na Tz hizi. Mwenzako kima cha chini si chini ya 10 Usd kwa saa hilo hutaki kulinganisha. Ana unemployment benefits wewe una Mfuko wa TASAF ambao ni msaada na haudelivi.
 
ACHA USHABIKI MKUU. Mimi ndani ya siku Tano hizi nimefanya miamala ya kibenki mara tatu kutuma pesa ya kiawango cha zaidi ya laki moja. Unajua nimekatwa tozo kiasi gani? 😡
 
Kampuni zinalipa kodi ni kweli? Hiyo pesa wanaikata kwenye nini? kwenye faida baada ya kampuni kupata faida.
Tena hizi kampuni za kigeni zina msamaha wa kodi( Tax relief), ulisikia lini mfanyakazi ana msamaha wa kodi? uliona wapi wananchi wamesamehewa kodi zao?

Kampuni zinaondoa kiwango kikubwa cha pesa kwa kutumia mfumo wa depreciation na non discrimination service kama chai ya Asubuhi. au chakula cha mchana.

Kampuni nyingi ile Net profit inayotakiwa kukatwa kodi inakuwa imepungua mno, kwa kutumia mbinu ya Tax evasion, Hivyo usielezee jambo usilolijua.

Kampuni nyingi zinatunza kiwango kikubwa cha pesa kama kama Reserve hivyo kukwepa kukatwa Umemzungumzia Mwanahisa(shareholder) ambaye anapokea gawio(Divinded) huyu yupo liable kulipa withholding tax kwa kuern pesa kutokana na uwekezaji wake na sio double taxation.

mkuu hivi unafahamu maana ya double taxation kweli? unafahamu sheria ya Tz na kimataifa haziruhusu jambo hili, kwa nini huoni ni tatizo?

Itakuwa mlamba asali wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…