Kwanini Nchi isiandae mashindano ya kimataifa?

Kwanini Nchi isiandae mashindano ya kimataifa?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Ukitazama Mikataba ya Azam TV kwa mpira wa Tz unaona kabisa mabilioni mengi yanawekeza kwenye mpira wa Simba na Yanga tu...

Wakati zipo nchi hazina uwekezaji huo lakini zinaaandaa michuano ya kimataifa..

Kwanini hatufikirii kuandaa
Africa nations cup?
Au world cup under 20?

Au common wealth games?

Au intercontinental Cup?..

Women world cup??

World club championship?

Nafikiri imefika wakati sasa tuanze kufikiria mambo yatakayo leta faida kwa nchi kiujumla kuliko huu mpira wa Manara na Mzee Mpili.

Serikali isihirikiane na wawekezaji binafsi kama Azam kuandaa baadhi ya michezo ya kimataifa tupate faida ya kweli..
 
Serekali ya Tanzania ni Utopolo. Daima hawawezakuwa na fikra kama hizo
 
Viwanja hatuna na uwezo wa kuanza kuviboresha kwa mkupuo hapo ndio penye changamoto. Kati ya majiji yetu ni dar pekee ndio kuna viwanja bora kwingine hamna kitu.

Fikiria una mashindano yanayohusisha timu hata 8 je hizo timu zitafanyia wapi training? Taifa halina viwanja bora vya kutosha pia Klabu zetu hazina training centre za kisasa ambazo zingeweza kutumika kwenye mashindano yaliyoandaliwa kitaifa.
 
Ndo tuwekeze kwa faida
 
Viwanja ndio shida. Kuandaa mashindano na wateja pia shida kama hamna simba na yanga katika hayo mashindano uliyoyasema.

Na simba na yanga zinapendwa na wawekezaji kama azam sababu zina mashabiki wengi wasio na kazi za kufanya.. hawa watu ni wateja wa content.

Azam anatumia mbinu ya msanii diamond. Ukitaka upate faida haraka tz .Weka content ambazo waswahili wanazipenda.. weka contenyt za umbea ama weka content za simba na yanga. Hela yako haipotei lazima upate faida kubwa
 
Hatujawahi wekeza huko kwingineko tukaona inashindikana..
 
Tanzania kuandaa mashindano ya kimataifa bado sana, labda yaandaliwe ila game zote zichezwe Dsm, miundombinu yetu hasa viwanja bado.

Huo mkataba wa Azam Media na Yanga na mingine ya aina hiyo wawekezaji huangalia faida kutoka kwa mashabiki wa hizo timu kubwa, lakini kwa timu ya taifa ni kamari, watanzania hatuna mapenzi sana kwa timu yetu ukilinganisha na vilabu vikubwa viwili.
 
Mambo hatukidhi vigezo kwenye mambo mengi...
 
Siasa ndio inaongoza mipango yote.

Mtoa hela anaona kabisa ROI itabebwa na wahuni.
 
Back
Top Bottom