Kwanini nchi ya Rwanda imeendelea kuliko Mkoa wa Kagera?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Habari wa ndugu. Ni swala ambalo liko wazi kuwa nchi ya Rwanda imeendelea kwa vipimo vingi ukilinganisha na mkoa wa Kagera. Hizi sehemu mbili zimepakana na hali ya hewa na mambo mengine wanafanana kwa karibu sana. Lakini ukiangalia sehemu hizi mbili utaona kama Kagera ina Advantage ya kuwa imeendelea kuliko Rwanda.

Rwanda ina eneo la kilomita za mraba 26,000 wakati Kagera ina eneo la kmsq 35,000. Hivyo Kagera ni kubwa kuliko Rwanda.

Pili, Rwanda ina watu 12m wakati Kagera ina watu 3m hivi. Tukumbuke kuwa kwa sehemu kubwa sehemu hizi zinategemea ichumi wa kilimo na wakazi wake wengi ni wakulima. Ukiangalia hizo takwimu utaona kuwa wananchi wa Kagera wana eneo kubwa zaidi la kulima na kufuga. Kama mtu mmoja ana ekari moja Rwanda, yule wa Kagera ana ekari Tano. Pia Kagera ina faida nyingine ya kuwa na ziwa kubwa kabisa, nadhani Kagera ndiyo inashare kubwa ya shoreline ya ziwa Viktoria. Na wakati huohuo watu wa Kagera wana access ya soko la watu milioni 60 kuuza bidhaa zao bila vikwazo vyovyote.

Tulisikia kuwa umoja ni nguvu, sasa kwanini Kagera iliyo katika nchi iwe na maendeleo duni kuliko Rwanda ambayo kihistoria ni kama imejitenga na nchi ya Tz? Je Rwanda ingekuwa mkoa wa Tanzania ingeweza kuwa na maendeleo iliyonayo? Je Kagera ingekuwa nchi ingefanana maendeleo na Rwanda au hata kuipita?
 
Mimi nadhani sababu kubwa ni kwamba Rwanda ni Nchi na Kagera ni mkoa ndani ya nchi ya Tanzania, hivyo hata kwenye ukusanyaji na mgawanyo wa mapato Kagera haijiendeshi yenyewe inategemea maamuzi kutoka serikali kuu, Kagera inaweza ikawa ni sawa na Rwanda kwa ukubwa lakini namna sehemu hizi mbili zinaendeshwa ni tofauti kabisa.
 
Kwahiyo mkuu kuna guarantee kuwa iwapo mkoa wa Kagera ungekuwa nchi ungekuwa na uchumi mkubwa kuliko Rwanda, tukiangalia kigezo hicho cha kujiendesha? au Kagera wakipewa some autonomy inaweza kuwa hivyo?
 
kwahiyo mkuu kuna guarantee kuwa iwapo mkoa wa Kagera ungekuwa nchi ungekuwa na uchumi mkubwa kuliko Rwanda, tukiangalia kigezo hicho cha kujiendesha? au Kagera wakipewa some autonomy inaweza kuwa hivyo?
Mimi naamini inawezekana kabisa vivyo hivyo kwa Zanzibar... lakini pia itategemea na aida gani ya uongozi utakaokuwepo madarakani.
 

This is an excellent observation. And for those in favor of the decentralized government, they can apply a comparative analysis like this one to make a compelling argument. Rwanda is a sovereign state. As such, structurally the government of Rwanda is set up to tackle a number of important issues which aren't in the rim of any regional administration in Tanzania. For example, in education sector, the government of Rwanda is responsible for higher education. So it builds and runs higher learning institutions. Whereas, in Tanzania, the best a regional administrator can do is to run secondary schools. Perhaps, if Kagera was an autonomy region, we could have a different story.

Apart from that, there's an issue patterning to the degree of separation between those at the top and those at the bottom of the political ladder. Rwanda is a compact country and the degree of separation isn't that vast. Stated differently, the president of Rwanda isn't that far from ordinary citizens and their issues. For example, in a single day, he can cruise from east to the west and see at first hand what has to be done. On contrary, the important decision maker in Tanzania doesn't have that luxury.

That said, the infrastructure in Tanzania is improving greatly so is the number of Tanzanians with disposal income. So in the near future, Kagera will match Rwanda in every measurable term. As a matter of fact, it might be even sweeter to live in Kagera than in Rwanda. Take for example its location. It's very close to major airports (Mwanza, Entebbe, Kigali, Chatto).
 
mchango mzuri sana mkuu, shukrani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…