Kwanini neno "Kilaza" linawekewa ****** humu JF

Kutwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2016
Posts
238
Reaction score
717
Habari wakuu,

Hivi hili neno Kilaza lilizoeleka kutumika vizuri tu kumuwakilisha mtu asiye na maarifa fulani huku akijifanya maarifa hayo anayo. Kinachonishangaza neno hili limekuwa likitumika kama tusi kubwa sana jukwaani kwa siku za hivi karibuni.

Najua kuna baadhi ya watu hutakiwi kulitumia kuwawakilisha wao ila hata humuhumu na id zetu unakuta mtu akitaka kulitumia anaweka dot(.) katikati mfano kila.za au kil.aza nk. wengine wanaweka ****** na ukishakutana na hizo nyota sita hapo unajua kabisa jamaa kaitwa Kilaza.

Je mods wanatoa ban ukitumia neno "Kilaza" kama lilivyo au.
Halafu kuna ndugu zetu wale wa Kilimanjaro ambao hili jina wengine unakuta ni la ukoo kabisa kama la yule ambaye chimbuko la hili jina lilipatikana tutakuwa tunawaita na Mr. ****** kweli.

Tuwape uhuru na wengine neno kilaza litumike tu vizuri panapostahili. Tuwapeni uhuru na wenye majina yao mbona matusi ya kuwekewa * yanajulikama wakuu.

Nawasilisha.
 
Mmh sas wew unatupa maswali yasiyoeleweka ***** ndo nin?
 
Niliandika "Kil.a.za" katika tittle na hata katika maelezo yangu ila nimegundua JF yenyewe ndiyo inafanya autocorrection ukiliandika lile neno kama lilivyo yenyewe inaweka ****** . Ni JF ndio wanazingua.
Ngoja nihamie kwenye kundi la kuweka vi dot(.) tu hamna namna sasa.
 
L


Ha ha ha ata pu.mbavu. ww amia kwenye vidoti.
 
Yaani ukiliandika tu linakuwa nyota hahahaha
 
MATUSI NA MANENO KM JESSIKA
KI.LAZA
NA MENGINE AMBAYO MODS WANAONA HAYAFAI


MANENO YA KICHOCHEZI
 
duh tena hiyo n automatic yan ukiandika tu zmakuja star ase raha san najarbu tena kilaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…