SoC01 Kwanini ni muhimu sana kuajiriwa au kujitolea kwanza kabla ya kuanzisha Biashara yako

SoC01 Kwanini ni muhimu sana kuajiriwa au kujitolea kwanza kabla ya kuanzisha Biashara yako

Stories of Change - 2021 Competition

odaafrica

New Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
2
Reaction score
12
Tatizo la ajira linazidi kuwa janga kubwa sana afrika na dunia na soko la ajira zitazidi kuwa baya zaidi miaka kadhaa baadaye baada ya dunia kuendelea kuamini juu teknolojia ya roboti kuliko binadamu katika kufanya kazi kwa weledi , kulalamika tu kwamba tumesoma na hakuna ajira huku tukiendelea kukaa tu nyumabani haitoshi wala kutatua tatizo lenyewe

Sisi kama vijana tunapaswa kuondoa uzembe huu kwa kufanya jitihada za kuondokana na tatizo hili badala ya kusubiri matangazo ya ajira kutoka Serikalini ama sekta binafsi, dawa ya kuondokana na tatizo sugu la ajira ni kujiajiri wenyewe , lakini kabla ya kujiajili wenyewe kuna jambo muhimu tunapaswa kufanya, kujiuliza maswali yafuatayo

  1. Je, tunaijua sekta binafsi vizuri?
  2. Katika sekta binafsi ni idara gani ungependa kujiajili huko mfano sekta ya afya, usafirishaji na uchukuzi, fasheni, kilimo, teknlojia, udalali, uuzaji wa chakula nk?
  3. Lakini je unaifahamu sekta hiyo vizuri? maana kila sekta ina lugha zake kwa kutoijua vizuri kunaweza kukufanya ujifunze kwa gharama kubwa ambayo inaweza hata kuharibu misingi ya maisha yako?
Ukiona unashindwa kuyajibu maswali hayo kwa ufasaha basi jua hauko tayari kupambana katika sekta binafsi maana huku hakuna huruma, kutokujua kwako ndiyo faida kwa mshindani wako na kukutoa kwenye mfumo wa sekta hiyo, hivyo basi nini cha kufanya ?

Unapokuwa na ndoto ya kujiajiri katika sekta binafsi basi ijue kiundani na unawezaje kuijua kiundani?

Njia ya kwanza kabisa hakikisha unasoma nakala mbalimbali zinazohusiana na diara yako , iwe vitabu ama kupitia internet ila jambo la pili na kubwa zaidi nenda kaombe kujitolea kwenye taasisi yeyote kubwa inayofanya vizuri katika idara hiyo ili kupata muda wa kujifunza kwa vitendo , kuwajua wateja na tabia zao , kuongeza wigo wa network yako pindi utakapo kuwa tayari kujiajili mwenyewe.

Kampuni nyingi binafsi na kubwa zina programu maalumu ( internship ) kwaajiri ya watu wanaotaka kujitolea kufanya kazi katika taasisi zao , na wengi wao hufika mbali zaidi na kuwalipa , ktk program hizo utajifunza mambo mengi sana kama vile:
  1. Jinsi taasisi kubwa zinavyoundwa (company structures)
  2. Jinsi ya kuajiri
  3. Mifumo wanayotumia, namna ya kusimamia matawi na wafanyakazi waliombali
  4. Jinsi ya kutengeneza mahusiano ya kudumu kati ya mteja na biashara yako
  5. Jinsi biashara zinavyolipa kodi
Baada ya hapo naamini utakuwa tayari kuanza safari yake ya ujasiliamali na kujiajili , hupaswi kuwa na haraka ni lazima usome na kujifunza kwanza kabla ya kuingia miguu yote , kila raheli katika safari yako ya kujiajiri na kujifunza.

quote-entrepreneurship-is-the-cornerstone-to-african-development-and-the-key-to-local-value-to...jpg
 
Upvote 11
Haya maswali ndiyo yanafanya watu wasitoke na kuanza kufanya kwa vitendo.
 
Tatuzo kubwa la vijana wanatoka vyuoni wakiwa na ndoto kubwa na tamaa ya mishahara mikubwa ikiwatawala...
Kujitokea kuna faida zaidi kuliko wengi wanavyo dhania, ikiwa kupata uzowefu kazini na pia wanao kuzunguka kupata nafasi ya kukujua/kukufaham vizuri
 
Nakusupport kwa asilimia fulani mleta mada, kwa hali yetu ya elimu inaonekana baada ya mtu kumaliza elimu yake bado anakuwa anakosa msingi mzuri wa ujuzi wa vitendo unaoweza kumwezesha kujua jinsi vitu katika ulimwengu wa uzalishaji, biashara au uendeshaji wa kampuni vinavyoenda na hivyo kujikuta anaanza kwa kutembea gizani, kupapasa na kuanza kutumia nguvu nyingi kugundua kanuni ambazo zimeshagundulika na karne na karne, kanuni za kipi cha kufanya au kutofanya katika biashara na mwisho wake anajikuta katika mchezo wa bahati nasibu ambao muda mwingi hufanya atumie nguvu nyingi mahali pasipo sahihi na mwisho wa siku kufeli na kukata tamaa. Kuna haja ya kuiendeleza elimu yetu ikae kivitendo zaidi, elimu ya vitendo ni muhimu sana katika sekta yoyote inayozalisha au kuongeza thamani.

Kuajiriwa au kujitolea ni njia kubwa kwa sasa ya kuweza kupata ujuzi huu wa vitendo ambao wengi tunakosa lakini sio lazima iwe njia pekee, kuna kitu kinachofanya watoto waliokulia kwenye familia za wafanya biashara waweze kuingia katika biashara kwa urahisi kuliko familia za waajiriwa, inabidi ifike wakati tuanze kujenga msingi kuanzia chini, sawa kizazi chetu bado kinapambana na changamoto za ajira na kama takwimu zinavyoonesha hakuna tumaini katika siku zijazo lakini baadhi yetu (iwe kwa makusudi au kutojali) wakifanikiwa tunasahau wengine wanaohitaji kushikwa mkono kwa upande wa kujua njia zipi na zipi za kupita, badala yake experience alizopata mtu anapotea nazo anapoondoka na kuacha wengine waanze upya pale pale alipoanza yeye, hii inafanya spidi yetu katika maendeleo, uzalishaji na uendeshaji wa biashara ibaki pale pale bila kuendelea kwa sababu kila mtu anayeanza anaanza chini kabisa badala ya kutumia experience zilizokwisha patikana na waliomtangulia.

Kuna haja ya kuchukua uamuzi sisi wenyewe kama vijana badala ya kulaumu mfumo uliopo kwani nikiwa mkweli kwa elimu tulionayo na misingi iliyowekwa ya masomo, njia ufundishaji na wafundishaji bado haiwezi kutusaidia kwa namna ilivyo sasa hivi, inabidi tufanye jitihada binafsi za kupambania ujuzi huu wa elimu ya vitendo, kuchanganya na ubunifu wetu wenyewe kuja na vitu vipya na kurithisha wale wanaokuja nyuma yetu wapate sehemu ya kuanzia ili waendeleze tutakapoishia na kuzidi kusukuma gurudumu vile vile kurithisha wale wanaowafuata pia.
Ni kwa njia hii ya kuwafikiria wanaotufuata nyuma yetu pia tutaweza kuevolve kwa haraka zaidi kuliko kuangalia tu kila siku ulimwengu unavyoenda kwa kasi hali sisi tupo pale pale tunapambana na matatizo yale yale.
 
Back
Top Bottom