Uchaguzi 2020 Kwanini ni Prof. Ibrahim Haruna Lipumba?

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234

Kwanini ni Prof Lipumba
1. Ni kwa sababu ana majibu ya kitaalam ya kutatua matatizo yanayo ikabili nchi na wananchi kwa ujumla

2. (i)Ana deni kwa watanzania linalotokana na kodi zao zilizotumika kumpa elimu na maarifa makubwa yaliyo na majibu ya kweli ya kutatua kero za umasikini wa wananchi walizodumu nazo kwa muda mrefu tangu kupata uhuru.

(ii)Ana deni kwa muumba wake kwa tunu aliyomjaalia ya kiwango cha juu cha ujuzi na maarifa makubwa yanayohusu majibu ya hakika ya kuondoa umasikini kwa wana nchi na Tanzania kwa ujumla wake

*kwani bila urais hawezi kutatua kero hizo?*
(i)Bila urais hawezi kutatua kero kutokana na mfumo wa nchi yetu ,mfumo ambao mtu akiwa rais yeye ndiye mwenye maamuzi ya nini kifanyike wapi na lini

(ii) Bila urais hawezi kwa sababu Mifumo kama hii siyo rafiki kwa maslahi mapana ya nchi na watu wake ndio maana CUF ina sema pamoja na mambo mengine itakayofanya ni pamoja na kujenga taasisi ya urais ili ifanye kazi kwa kuzingatia miongozo ya Nchi badala ya mtu mmoja kama afanyavyo mheshimiwa Rais wetu na kama walivyofanya watangulizi wake

(iii)Kufanikisha yote hayo CUF italazimika kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili iweze kujenga mifumo imara ya uongozi na utawala BORA isiyokuwa ya kishabiki ila weledi.

(iv) mifumo hiyo inatarajiwa iweze kujibu kiu ya wananchi ya kuweza kusimamia nchi yao

(V)Nchi ikiwa na taasisi ya urais itaweza kukusanya wale wote waliyotunukiwa taaluma na maarifa mbalimbali ili kuweza kutowa majibu mbalimbali ya changamoto zilizopo na zitakazojitokeza

3. *Hofu ya Prof ya kukosa majibu ya maswali atakayokutana nayo kwa mola wake ndio yanayomsukuma kuendelea kuwaonesha Wananchi kwamba kuna jambo ambalo hajafanya kwao na kwamba wasipo liona wao yeye atakuwa amefanya jitihada ambazo sisi wana wa nchi tumeziona yeye amedhihirisha na Muumba wake amezishuhudia juhudi zake hizo.*

4. Prof kasaidia Nchi nyingi kujikwamua kiuchumi na ni miongoni mwa magwiji walioandaa malengo ya maendeleo ya Milenia hivyo anajua mapito sahihi ya kupita ili kufika huko kwenye MDGS( MILLENNIUM DEVELOPMENT GOALS)
 
Tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995 hadi leo (25yrs) kila uchaguzi mkuu lazima agombee na matokeo anayopata ni kichekesho ila yupo tu! Oneni hata aibu. Au ndio hivyo yasemwayo kwamba yupo kwenye mission maalumu?
 
Hivi sababu ya yeye kujivu uenyekiti ni ili, baadae arudi tena?
 
Ni kweli kiongozi, lakini binafsi naona mhe. Prof lipumba angejaribu kutuachia vijana tuipeperushe bendera ya chama.
Huu ndo ukomavu wa siasa toka miaka ya 90's anagombea URAIS. Wanacuf na wadau wengine wa siasa ebu liangalieni ili kwanza.

Mhe Prof ni mbobezi wa elimu ya juu kuhusu masuala mazima ya uchumi.

NAPENDA kumuhuliza swali mheshimiwa mbona hatuone maendeleo au harakat zozote za kimaendeleo katika chama chake?

Na je toka miaka hiyo bado yupo kwenye siasa anashindwaje kuachia ngazi chama kiendeshwe na mwenyekiti mwingine?

Au vijana wazalendo wa chama hawapo?
 
Anejishushia sana heshima yake...
Wastage of resources. Kama kweli angekua that smart angejua kwamba yeye sio maarufu tena, hauziki kisiasa kwasababu hakubaliki na watu. Angeendelea tu na shughuli zake zinazohusiana na taaluma iliyompa Uprofesa

Kadri chama chake na yeye mwenyewe wanavyozidi kulazimisha agombee Urais ndivyo anavyozidi kupoteza hadhi na heshima yake kidogo iliyobakia
 
Professor uchwara ..apumzike tu Siasa maana ni msaliti
 
Huyu ndio ana ukurasa sahihi wa upinzani nchini. Hawa ndio wanaipa ushindi mwepesi CCM mwaka huu kwa sababu ya mambo yao ya 2015 na Lowassa na Mbowe!
 
Bora huyu mzee angepeprusha bendera ya ccm angalao anajua kumwaga sera japo za kitapeli yule wa ccm hata kiswahili hajui kiingereza hajui anafanya kampeni kwa lugha za Wajomba zake wasukuma
 
ha ha haaaaaa jamani nashindwa hata kukoment
 
Hili kituko mnaleta huku ya nini kama siyo kutupotezea mda kulijadili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…