olimpio
JF-Expert Member
- Apr 5, 2023
- 418
- 866
Kwa muda mrefu sasa ,serikali imekua ikitoa matamko kua inataka watanzania watambulike kwa utambulisho sahihi , kwa nchi yetu Tanzania NIDA wamejitahidi sana tumepata vitambulisho karibu asilimia kubwa ya Watanzania.
Kinachofanyika kwa sasa ,kampuni yeyote ikitaka kufanya name verification(uhakiki wa majina au utambulisho wa mtu) inalazimika kulipa 500 TZS kwa kila ombi(request) , mfano mtu anaposajili line ya simu makampuni ya simu yanalazimika kulipa 500 kwa kila uhakiki wanaoufanya NIDA, Makampuni mengine ya serikali na binafsi yanayotaka kuhakiki watanzania wanaojisajili au wanaotaka kupata huduma kwao lazima walipe 500 kwa kila ombi NIDA.
Hii maana yake ni nini?
Kampuni ya simu inayosajili wateja laki moja(100k) inalipa inalipa 50M (Millioni Hamsini), kibiashara hii inamaanisha Makampuni haya yatatafuta namna kulipia hizo gharama kwenye vifurushi vinavyouzwa
Kwa taasisi za serikali na binafsi nyingine zinalazimika kuachana na zoezi la kuhakiki kwani linawaingizia gharama kubwa sana.
Maswali fikirishi
1. Kama watanzania tunalipa kodi ,kwa nini NIDA wanatoza pesa kuhakiki taarifa ambazo tumewapa sisi wananchi?
2. Kama NIDA wanashida ya pesa ,kwa nini serikali isiwape ruzuku?
3. Kwanini mzigo huu tunawarudishia wananchi kupitia gharama za makampuni yanayohakiki taarifa?
4. Kama NIDA wanauza taarifa zetu kwa namna hio ,sisi wananchi wanatulipa nini in return?
5. NIDA hawaoni kua kulipisha uhakiki wa vitambulisho unafanya watu waendelee kutoona umuhimu wa kutumia vitambulisho?
6. Kama wanalipisha kuogopa taasisi zisitumie vibaya huduma hio ,kwa nini wasiweke control mechanism nyingine tofauti na kulipisha?
Mwisho
Tunaua innovation kwa kuweka vigingi visivyo na maana , server za NIDA ni za Umma ,hawanunui kwa pesa zao mfukoni ,wasitoe gawio wanunue server na kulipia gharama za uendeshaji wa mfumo wa NIDA lakini wasitulipishe wananchi, taarifa ni zetu hatutaki mziuze