Kwanini Nigeria wameweza sisi tunajiumauma?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Nigeria to review privatisations

 
Huenda sisi ni wazito kufikiri, la sivyo ni wazito kuamua!
God bless us!
 
Huenda sisi ni wazito kufikiri, la sivyo ni wazito kuamua!
God bless us!

Mkapa aliposema sisi ni wavivu wa kufikiri tuliona anatutukana, sasa wenyewe tumeanza kung'amua taratibu. Lakini ni obvious kuwa kuna wanaopenda hali hiyo, kwa sababu inatoa loop holes za kuiba.
 
Sisi tunaamini bila wazungu hatuwezi kufanya kitu, muulize FMES!
 
Sisi ndivyo tulivyo....hata huko Nigeria ni magirini tu hakuna lolote la maana litakalotokea
 
Nakumbuka huko nyuma mara baada ya Mazungumzo ya Habari kulikuwa na kile kilichoitwa "Ujinga wa Mwafrika"... na kulikuwa na vijitabu pia... hatimaye vilipigwa marufuku. Nadhani kuna haja ya kuviandika tena.
 
Wengine hatukuvisoma hivyo....vilikuwa vinazungumzia ujinga upi? Kwa nini vilipigwa marufuku na nani alivipiga marufuku?
 
Tofauti yetu wenzetu wana mafuta na vichwa vigumu...sisi tuna amani na utulivu na ujinga usiokoma.
 
Nyani, vijitabu hivi vilikuwa viko katika mfululizo (vya kijani, nyekundu...) na ndani yake kulikuwa na hadithi/visa fupi fupi za waafrika wakati wa Ukoloni au walivyohusiana na wakoloni. Vilikuwa vinaelezea kwa mfano ilikuwaje siku mwafrika alipoona baiskeli, alivyoletewa suruali, alivyoona motokali etc

lengo lilikuwa ni kuonesha kuwa ujinga hutoka; vilikuwa vinachekesha sana. Hata hivyo mwisho wa kila kisa kulikuwa na funzo fulani la kimaadili au kimtazamo.
 
Okay...I hope vitarudishwa kwani tunahitaji hayo mafunzo
 
Mimi bado ninavyo viwili vimechakaa chakaa hivi, ukivisoma utacheka sana na kujiuma vidole vilevile!
 
Mwanakijiji vipi simu umezima, Soma PM yako pia plizi!

Nimekuachia message simu ya kazini!

Asante
 
J e usanii ni viongozi au wananchi? Maana naona ni wote. Leo hii tunapiga kelele kila kona ya nchi. Ahadi zilitolowa kisanii, watu wakaingia mkenge wakatoa kura kibao. Ngoja 2010 utaona the same History inajirudia watashinda tena kwa mbwembwe. Siju Watanzania tuna mdudu gani. I dont know what is wrong. KISA WAPIGA kura wanadanganywa ukipigia kura mtu mwingine MANI IATVUNJIKA NA WANAKUBALI. Nigerians soma History yao na character yao they are high risk takers katika nyanja zote za maisha! kuanzia miaka ya 60 mpaka 80 wamakuwa na serikali zaa kijeshi. They know! sisemi nasi tuende huko la. In nature Wana wa Tanzania ni wapole sana hasa WATANGANYIKA. Tukubali tusikubali vizazi vijavyo vitakuja tulaumu tulikuwa tunafanya maamuzi ya aina gani. mikataba yote si misahafu au biblia. therefore if fake revoke them! lakini nani? kiongozi mlafi na mwenye Njaa ya Mali??? Who will do it? Tumekwisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…