Kwanini Nishati ya Nyuklia ni janga la kitaifa

Kwanini Nishati ya Nyuklia ni janga la kitaifa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Wanasiasa wamekuwa wakipigia baragumu la nguvu wakitetea uvunaji wa Uranium kwa matumizi ya uzalishaji wa nishati ya nuklia kwa kututupia peremende zifuatazo:-

1) ndiyo ufumbuzi wa kudumu wa kiu yetu ya muda mrefu ya kujitosheleza kwenye mahitaji yetu ya nishati hapa nchini.

2) Eti ni nafuu sana!

3) Inapatikana nchini hivyo siyo mzigo wa kiu ya fedha za kigeni bali itakuwa na msaada mkubwa wa kuzalisha fedha za kigeni kwa kuuza nishati ziada kwa majirani zetu.

4) Ajira lukuki kwa vijana wetu.

5) Utaalamu wetu kwenye fani husika utakua maradufu!

6) Kuzalisha maeneo ya machimbo na kupunguza misuguano kati ya Dar na mikoa ya pembezoni. Hivyo kuharakisha maendeleo yanayowiana.

Hoja hizi na nyinginezo nyingi hazina makalio kabisa kwa sababu zifuatazo:-

1) Gharama za miundo mbinu na uendeshaji wake zinategemea mikopo ambayo serikali yetu ndiyo itatoa dhamana kwa maana ikishindikana kulipwa basi nchi nzima kubebeshwa mikopo hiyo. Tatizo kubwa ni kuwa mikopo hiyo hailipiki kutokana na tozo kubwa za riba kwa sababu mabenki huona ina hatari (risks) nyingi na kubwa. Kutokana na ukubwa wa tozo za riba nchi kamwe haiwezi kuirudisha na hivyo kuwa mzigo mkubwa kwa taifa.

2) Uchafuzi wa mazingira na kuongeza kasi ya magonjwa ya saratani kwa raia ambao hawatanufaika moja kwa moja na miradi tajwa.

3) Athari za kimazingira kuwagusa wengi ambao hawatanufaika moja kwa moja na miradi hiyo na hakuna miundo mbinu ya kuhakikisha wanafidiwa ipasavyo.

4) Uchafu unaozalishwa na mitambo ya umeme wa nuklia hatuna mkakati wa kuuthibiti na gharama za kuuthibiti zinazidi faida tarajiwa.

5) Kutokana na gharama za kununua umeme kuendelea kukua kwa mithili isiyoelezeka ni dhahiri ya kuwa watanzania wengi ambao ni wa kipato cha chini watashindwa kumudu gharama zake hivyo kuwa waangalia kideo ambacho kiko nje ya uwezo wao!

6) Matukio ya ugaidi yamethibitika kuwa nje ya uwezo wetu wa kuyathibiti na mkakati wetu kuishia kuwa ni wa zimamoto. Mitambo hii itakuwa yenye mvuto mkali kwa magaidi ambao wana malengo ya kuturudisha nyuma. Mitambo hii kama ikilipuliwa athari zake za kimazingira zitakuwa juu sana na uwezo wetu wa kuyasafisha mazingira ni mdogo na hivyo kuhatarisha afya zetu bila sababu ya msingi.

7) Ajali za mitambo ya namna hii kule Urusi-"Chernobyl" na hivi karibuni kule Japan ..Fukushima, zinatufunza ya kuwa pamoja na nchi tajwa kuwa na uzoefu mkubwa kwenye taaluma hii ya nuklia matukio ya ajali kwenye mitambo husika haina kinga na gharama zake kuendelea kusikika miaka mingi baada ya ajali zenyewe kutokea...

8) http://www.earthtimes.org/newsimage/japanese-nuclear-disaster-tip-iceberg_44.jpg
 
Back
Top Bottom