Kwanini Nyerere aliachia madaraka mapema?

Smile

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
15,347
Reaction score
11,619
HELO GREAT THINKERS
NAOMBENI MNIKARIBISHE HUMU LEO NIMEWEKA MAMBO YA MAPENZI PEMBENI.
NAOMBENI MNIJIBU
KWANINI MZEE WETU NYERERE ALIACHIA MADARAKA MAPEMA BAADA YA KUTOA KATIKA MIKONO YA MKOLONI?
KWANINI HAKUKAA KAMA WENZAKE kina Mugabe wanaodai hawajaona watu wenye uwezo wa kuwaachia nchi.au mzee wetu aliona yeye hawezi tena na wanaoweza kuongoza wapo awaachie? ni nini sababu ?
pia je alikuwa na vision gani kwa warithi wake au aliachia tu ? je hayo maamuzi yalikuwa sahihi/yalikuwa na tija kwa taifa ama?sielewi sielewi naombeni mnijibu
nawasilisha
wenu mtiifu smile
 
mimi nahisi alisoma alama za nyakati ndio maana akang'atuka mapema wewe si unafahamu yaliyowakuta kina obote pale uganda nadhani ndicho kilichomkimbiza na chengine mambo ya kubadili mifumo ya uchumi kutoka ujamaa mpaka mchanganyiko wa ujamaa na ubepali.
upo hapo mkuu smile..
 
Nyerere aliachia madaraka kwasababu ya mapenzi ya nchi yake; hakutaka kuingiza nchi kwenye shida zisizokuwa na msingi kama vile machafuko ya amani!! Kikwete angekuwa na mapenzi ya Tanzania kama Nyerere angeachia mwingine aongoze nchi badala ya kuwaacha wananchi wanateseka kwasababu ya kutokuwa na uwezo wa kuongoza.
 
kwani hapa tz kuna mtu mwenye jeuri ya mapinduzi mkuu? alihofia hilo kwa nini?
 
Nyerere aliachia madaraka kwasababu ya mapenzi ya nchi yake; hakutaka kuingiza nchi kwenye shida zisizokuwa na msingi kama vile machafuko ya amani!! Kikwete angekuwa na mapenzi ya Tanzania kama Nyerere angeachia mwingine aongoze nchi badala ya kuwaacha wananchi wanateseka kwasababu ya kutokuwa na uwezo wa kuongoza.
kwa hiyo ni uoga ulimkimbiza ikulu?
 
Mbona hamnijibu?
 
kwa hiyo ni uoga ulimkimbiza ikulu?
Uoga gani unaozungumzia wewe? Nyerere hakuwa chifu na kumbuka alifuta mfumo wa machifu. Kuna wakati wana TANU walimwomba atangazwe President for life kama alivyokuwa Banda akawafokea kweli kweli.
 
HELO GREAT THINKERS
NAOMBENI MNIKARIBISHE HUMU LEO NIMEWEKA MAMBO YA MAPENZI PEMBENI.
NAOMBENI MNIJIBU
KWANINI MZEE WETU NYERERE ALIACHIA MADARAKA MAPEMA BAADA YA KUTOA KATIKA MIKONO YA MKOLONI?
KWANINI HAKUKAA KAMA WENZAKE kina Mugabe wanaodai hawajaona watu wenye uwezo wa kuwaachia nchi.au mzee wetu aliona yeye hawezi tena na wanaoweza kuongoza wapo awaachie? ni nini sababu ?
pia je alikuwa na vision gani kwa warithi wake au aliachia tu ? je hayo maamuzi yalikuwa sahihi/yalikuwa na tija kwa taifa ama?sielewi sielewi naombeni mnijibu
nawasilisha
wenu mtiifu smile

Smile,

Kusema ukweli Nyerere hakuachia Madaraka mapema. Miaka 23 si mchezo. Pamoja na hayo hakutaka kukaa madarakani muda wote huo.

Mwanzano mwa 70 lilitokea pendekezo la kumfanya kuwa rais wa maisha kama Kenyatta. Lakini akakataa na kupanga kuachia kati 1975 au 1980.

Mwaka 1980 uchumi ulikuwa ni mbaya na akaona kuwa kumwachia mtu mwingine isingekuwa fair. Hivyo akaendelea na kipindi cha 1980-1985 kwa mategemeo kuwa uchumi utakuwa mzuri. Lakini mambo yakaboronga. Hivyo ikabidi aachie.

Katika maamuzi aliyofanya sahihi kabisa ni yeye kuachia ngazi.
 
kwa hiyo ni uoga ulimkimbiza ikulu?

Smile, wanaoogopa kuitema Ikulu ni watu kama Mugabe, Wade etc, ambao wanajua wakitoka tu, mkono wa sheria utawafuata nyuma. Nyerere alikuwa JASIRI. Wote tunajua ugumu uliopo kuachia kitu kitamu kama madaraka.

Miongoni mwa maamuzi bora kabisa aliyofanya mzee JKN ni kuachia madaraka ili angalau apate muda na nafasi ya kumshauri anayechukua ili kutorudia baadhi ya makosa aliyoyafanya yeye.
 
Sio kweli kuwa wanaogopa sheria. Kuna viongozi wengine wanakaa madarakani kwa sababu wanaamini kuwa wao peke yao ndio wenye uwezo kutatua matatizo. Wengine wanakuwa addicted na madaraka.
 
Kama rafiki yetu Mu7
 
Kama rafiki yetu Mu7

Jasusi,

Kenyatta aliitwa baba wa taifa bado akiwa madarakani. Kama sitakosea Nyerere haku-entertain ubaba wa taifa na hata landmarks kupewa jina lake. Nakumbuka alikataa kiwanja kimoja cha michezo kupewa jina lake katika siku ya ufunguzi. Na wakakipa jina la Mandela.

Ilikuwaje baadaye alianza kukubali ubaba wa taifa?
 
Mandela anaweza kusema kaachia madaraka mapema.

Myerere kakaa miaka 23 kwenye power, huwezi kusema "kaachia madaraka mapema". Miaka 23 ni umri wa mtu aliyefikisha "age of majority" tayari.

Unachoweza kuuliza ni kwa nini aliachia madaraka bila ya kulazimika.

Jibu ni kwamba aliona kashindwa na kuendelea kungeharibu legacy yake kama "Philosopher King" akajua principle ya quit while you can, before the masses Causescu you brutally at the central square.
 
Zakumi,
Nyerere hakutaka kutukuzwa. Lakini pia ni mtu aliyeelewa sana historia. Nakumbuka siku za mwanzo wa uhuru walimwita majina ya ajabu ajabu, mtukufu, mheshimiwa, akayakataa yote akasema niiteni Mwalimu. Hili la baba wa taifa naona hakuwa na jinsi ya kulikataa kwa sababu alijua kwamba katika historia, kila taifa limekuwa na mzazi wake. Marekani alikuwa George Washington, Ufaransa alikuwa Napoleon, etc. etc.
 
Mandela anaweza kusema kaachia madaraka mapema.

Myerere kakaa miaka 23 kwenye power, huwezi kusema "kaachia madaraka mapema". Miaka 23 ni umri wa mtu aliyefikisha "age of majority" tayari.

Unachoweza kuuliza ni kwa nini aliachia madaraka bila ya kulazimika.

Jibu ni kwamba aliona kashindwa na kuendelea kungeharibu legacy yake kama "Philosopher King" akajua principle ya quit while you can, before the masses Causescu you brutally at the central square.
Kiranga,
Unachosema ni kweli. Lakini vile vile zingatia kwamba Mandela ameingia mamlakani umri umeshakwenda. Imagine kama angeingia mamlakani akiwa na umri ambao Castro alikuwa nao wakati anaingia Havana! Au kama Afrika Kusini ingepata uhuru mwaka 1964 badala ya 94? Je, angekaa tu mamlakani miaka mitano na kuachia ngazi? I think not.
 
Za-10 katoa majibu sahihi sana. Nyerere hakuachia madaraka mapema, alikaa madarakani kwa zaidi ya miaka 20; huo ni muda mrefu sanakwa kiongozi mwenye akili timamu kuendelea kuwapo madarakani ukitoa maamuzi makubwa ya kitaifa. Alikuwa anaplani kuachia madaraka mwaka 1980 baada ya kuunganisha TANu na ASP, na akafanya mojawapo ya majukumu yake katika kipindi cha 1975-1980 kuwa ni kuunganisha TANu na ASP, jambo ambalo lilikamilika mwaka 1977 chini ya usimamizi wa Pius Msekwa. Hata hivyo ile vita ya mwaka 1979 dhidi ya Amin iliharibu mambo mengi kiasi kuwa Nyerere alisema ataendelea kuyasimamia tena kwa miaka mingine mitano, ndiyo maana mwaka 1985 akaondoka ingawa alikuwa hajayanyoosha mambo hayo.
 
Uoga gani unaozungumzia wewe? Nyerere hakuwa chifu na kumbuka alifuta mfumo wa machifu. Kuna wakati wana TANU walimwomba atangazwe President for life kama alivyokuwa Banda akawafokea kweli kweli.
nashukuru kwa majibu yako mkuu lakini sijaridhika.mugabe alisema haWEZI KUACHIA MADARAKA KWANI HAONI MTU MWENYE UWEZO WA KUMUACHIA NCHI AONGOZE.HILI KWA UPANDE WETU UNAZUNGUMZIAJE MKUU? HAPA KWETU MRITHI WA MWALIMU ALIPATIKANA MAPEMA AU NI VP?
 
smile, wanaoogopa kuitema ikulu ni watu kama mugabe, wade etc, ambao wanajua wakitoka tu, mkono wa sheria utawafuata nyuma. Nyerere alikuwa jasiri. Wote tunajua ugumu uliopo kuachia kitu kitamu kama madaraka.

Miongoni mwa maamuzi bora kabisa aliyofanya mzee jkn ni kuachia madaraka ili angalau apate muda na nafasi ya kumshauri anayechukua ili kutorudia baadhi ya makosa aliyoyafanya yeye.
unavoona haya maamuzi yana impact gani kwetu leo mkuu?
 
Back
Top Bottom