kwani hapa tz kuna mtu mwenye jeuri ya mapinduzi mkuu? alihofia hilo kwa nini?mimi nahisi alisoma alama za nyakati ndio maana akang'atuka mapema wewe si unafahamu yaliyowakuta kina obote pale uganda nadhani ndicho kilichomkimbiza na chengine mambo ya kubadili mifumo ya uchumi kutoka ujamaa mpaka mchanganyiko wa ujamaa na ubepali.
upo hapo mkuu smile..
kwa hiyo ni uoga ulimkimbiza ikulu?Nyerere aliachia madaraka kwasababu ya mapenzi ya nchi yake; hakutaka kuingiza nchi kwenye shida zisizokuwa na msingi kama vile machafuko ya amani!! Kikwete angekuwa na mapenzi ya Tanzania kama Nyerere angeachia mwingine aongoze nchi badala ya kuwaacha wananchi wanateseka kwasababu ya kutokuwa na uwezo wa kuongoza.
Uoga gani unaozungumzia wewe? Nyerere hakuwa chifu na kumbuka alifuta mfumo wa machifu. Kuna wakati wana TANU walimwomba atangazwe President for life kama alivyokuwa Banda akawafokea kweli kweli.kwa hiyo ni uoga ulimkimbiza ikulu?
HELO GREAT THINKERS
NAOMBENI MNIKARIBISHE HUMU LEO NIMEWEKA MAMBO YA MAPENZI PEMBENI.
NAOMBENI MNIJIBU
KWANINI MZEE WETU NYERERE ALIACHIA MADARAKA MAPEMA BAADA YA KUTOA KATIKA MIKONO YA MKOLONI?
KWANINI HAKUKAA KAMA WENZAKE kina Mugabe wanaodai hawajaona watu wenye uwezo wa kuwaachia nchi.au mzee wetu aliona yeye hawezi tena na wanaoweza kuongoza wapo awaachie? ni nini sababu ?
pia je alikuwa na vision gani kwa warithi wake au aliachia tu ? je hayo maamuzi yalikuwa sahihi/yalikuwa na tija kwa taifa ama?sielewi sielewi naombeni mnijibu
nawasilisha
wenu mtiifu smile
kwa hiyo ni uoga ulimkimbiza ikulu?
kwa hiyo ni uoga ulimkimbiza ikulu?
Smile, wanaoogopa kuitema Ikulu ni watu kama Mugabe, Wade etc, ambao wanajua wakitoka tu, mkono wa sheria utawafuata nyuma. Nyerere alikuwa JASIRI. Wote tunajua ugumu uliopo kuachia kitu kitamu kama madaraka.
Miongoni mwa maamuzi bora kabisa aliyofanya mzee JKN ni kuachia madaraka ili angalau apate muda na nafasi ya kumshauri anayechukua ili kutorudia baadhi ya makosa aliyoyafanya yeye.
Kama rafiki yetu Mu7Sio kweli kuwa wanaogopa sheria. Kuna viongozi wengine wanakaa madarakani kwa sababu wanaamini kuwa wao peke yao ndio wenye uwezo kutatua matatizo. Wengine wanakuwa addicted na madaraka.
Kama rafiki yetu Mu7
Zakumi,Jasusi,
Kenyatta aliitwa baba wa taifa bado akiwa madarakani. Kama sitakosea Nyerere haku-entertain ubaba wa taifa na hata landmarks kupewa jina lake. Nakumbuka alikataa kiwanja kimoja cha michezo kupewa jina lake katika siku ya ufunguzi. Na wakakipa jina la Mandela.
Ilikuwaje baadaye alianza kukubali ubaba wa taifa?
Kiranga,Mandela anaweza kusema kaachia madaraka mapema.
Myerere kakaa miaka 23 kwenye power, huwezi kusema "kaachia madaraka mapema". Miaka 23 ni umri wa mtu aliyefikisha "age of majority" tayari.
Unachoweza kuuliza ni kwa nini aliachia madaraka bila ya kulazimika.
Jibu ni kwamba aliona kashindwa na kuendelea kungeharibu legacy yake kama "Philosopher King" akajua principle ya quit while you can, before the masses Causescu you brutally at the central square.
nashukuru kwa majibu yako mkuu lakini sijaridhika.mugabe alisema haWEZI KUACHIA MADARAKA KWANI HAONI MTU MWENYE UWEZO WA KUMUACHIA NCHI AONGOZE.HILI KWA UPANDE WETU UNAZUNGUMZIAJE MKUU? HAPA KWETU MRITHI WA MWALIMU ALIPATIKANA MAPEMA AU NI VP?Uoga gani unaozungumzia wewe? Nyerere hakuwa chifu na kumbuka alifuta mfumo wa machifu. Kuna wakati wana TANU walimwomba atangazwe President for life kama alivyokuwa Banda akawafokea kweli kweli.
unavoona haya maamuzi yana impact gani kwetu leo mkuu?smile, wanaoogopa kuitema ikulu ni watu kama mugabe, wade etc, ambao wanajua wakitoka tu, mkono wa sheria utawafuata nyuma. Nyerere alikuwa jasiri. Wote tunajua ugumu uliopo kuachia kitu kitamu kama madaraka.
Miongoni mwa maamuzi bora kabisa aliyofanya mzee jkn ni kuachia madaraka ili angalau apate muda na nafasi ya kumshauri anayechukua ili kutorudia baadhi ya makosa aliyoyafanya yeye.