wewe vipi? Nyerere alikuachieni utitiri wa vyuo vya elimu, kilimo, uvuvi, ufundi, uhasibu, utibabu, maji , usafirishaji, umeme, misitu, ufugaji, siasa, uandishi wa habari, biashara, utalii, ushirika, sanaa, ardhi, fedha nk nk. Huoni kuwa hata mlipoamua kuvipandisha daraja na kuviita Universties hamkupata tabu ya majengo wala logistics. Baada ya Nyerere nyie wapenda wasomi mmejenga vyuo vingapi zaidi ya kimoja tu UDOM? Kwa miaka 21 Nyerere alijenga utitiri wa vyuo, nyie wapenda wasomi kwa miaka 27 mmejenga chuo kimoja tu, huoni kwamba wewe ni kichekesho usiye na aibu wala adabu. Hii nchi watu walikuja toka nchi mbalimbali kuja kupata elimu, walitoka swaziland, lesotho, zambia, botswana, uganda, kenya, DRC etc jamani nyie msio fundishwa na mama zenu ni lini mtamwacha mzee wa watu apumzike .