Hii ni Chemistry ya kitaabibu, mechanism ni ndefu ila nitakuelekeza kwa ufupi.
Dawa unapomeza, ama kutundikiwa, inapenya kwa kufyonzwa na kuingia kwenye membrane mbali mbali za oragan na tissue, kisha kwenye mfumo Wa damu, hormone zinazohusika na mabadiliko ya mwili zinapokea nakupeleka sehemu husika(panapoumwa) lakini haimanisha dawa yote unayotumia inaenda sehemu moja, hapana, dawa zinasambazwa kwa kiwango kidogo kidogo kwenda kila sehemu ya mwili hadi pale itakapopata tatizo. Inagawanjwa katika viwango vidogovidogo sana ila sio lazima viwango vilingane.
Angalizo: Dawa yote unayitumia ingekuwa inaenda srhemu husika yenye tatizo maana yake mtu angekuwa anapona kwa muda mfupi na kwa kiwango kidogo cha dose. Kwakuwa inasambazwa hata sehemu nyingine ambazo haziumwi ndio maana mtu hupewa dawa atumie kwa siku kadhaa.
Tofauti na minyoo ambazo hukaa kwenye tumbo au utombo, mtu akipewa dawa zinaenda direct kukutana na wadudu na ndio maana dose yake ni simple.