Kwanini "Parachute" sio salama kwa ndege za abiria?

Alejandroz

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2017
Posts
329
Reaction score
413
Watu wengi wamekuwa wakiuliza swali.

"Kwanini ndege za abiria wasiweke miamvuli {parachutes} ili kila mtu aweze kuruka inapotokea dharura"

Kiuhalisia kwasasa haiwezekani kwasababu zifuatazo:

1> Urukaji kwa kutumia mwamvuli {parachute} unahitaji mafunzo ya saa 4 hadi 5 darasani ikifuatia vitendo akiwemo mwalimu mmoja au wawili.

Utuaji unahitaji akili na ustadi mkubwa ili kuepuka kuvunja viungo vya mwili.

Ndege zibebazo abiria 100 hadi 500 ni vigumu kutoa mafunzo gharama na muda.

2>Urukaji wa kawaida wa mwamvuli ndege haitakiwi kuzidi kasi ya 200km/saa na umbali usiozidi futi 13,000 kwa warukaji waliobobea na Futi 3,500 warukaji wa kawaida ukiacha urukaji maalumu wa kijasusi au kijeshi.
Ndege kama Boeing787 {Dreamliner} kawaida hupaa futi 35,000 hadi 43,000 kwa kasi inayofika hadi 900km/saa.

Kuruka katika kasi hiyo unaweza kuvunjwa na kusambaratishwa na upepo na kupigizwa katika mbawa au mkia wa ndege.

Urukaji wa mwamvuli unaozidi futi 13,000 unahitaji kifaa maalumu cha kukufahamisha kimo ulichopo, Musk na Mtungi wa 'oxygen' kwasababu umbali huo hakuna oksijeni ya kutosha hivyo unaweza kuzimia kwa kukosa hewa {hypoxia} kabla ya kufika kimo sahihi cha kufungua mwamvuli wako.

3> Mwamvuli mmoja na vifaa vyake vya kiufundi unaweza kugharimu kati ya milioni 15 hadi 20.

4> Mafunzo yanahitaji kufahamu kuendesha mwamvuli huo pamoja na ishara za mikono kama njia ya mawasiliano.

5>Mwamvuli mmoja una kilogramu zaidi ya 20, mara idadi ya abiria wote ni uzito mkubwa sana ambao utaathiri mafuta na uzito wa ndege.

6>Urukaji wa mwamvuli unahitaji kupeana nafasi hadi futi 500 au nusu dakika kwa watu wa kawaida ili kuepuka kuvaana angani.

Hii si rahisi kwa abiria walio'panic kwenye dharura.

7>Takwimu zinaonesha ndege nyingi asilimia 80% hupata dharura wakati wa kutua au kupaa.
Hivyo hakuna muda na kimo cha kutosha abiria kuweza kuruka.

8> Ndege chache zipatazo dharura katika kimo cha mbali husababishwa na hali mbaya ya hewa kama wingu la mawe na radi {thunderstorm} hivyo ni vigumu kuruka na mwamvuli katika hali hiyo.

9> Dharura nyingi zinahitaji ufunge mkanda kuepuka kurushwa au kuelea ndani ya ndege.

Kwahiyo ni vigumu kuvaa mwamvuli na kutembea kufikia mlango.

Pia ndege itahitaji mlango kuundwa na milango maalumu nyuma ya kutokea.

10> Ndege zipaazo kimo cha mbali huwa zinatengeneza mkandamizo wa hewa ndani {cabin_pressure} ili abiria apate mazingira yanayofanana na ardhini kuepusha damu kujaa gesi, kuchemka povu {blood_boiling_bubbles} na kukusababishia kifo kwasababu ya 'pressure' ndogo.

Kutulia ndani ya Ndege ni salama zaidi:

Source: Aviation Media Tanzania

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
SOmo zuri sana.
Kuna siku tulipata dhoruba ya hali ya hewa kuwa mbaya kutokana na mvua kubwa, nilifadhaika sana na kuwaza kama kuna uwezekano wa kuruka.
 
SOmo zuri sana.
Kuna siku tulipata dhoruba ya hali ya hewa kuwa mbaya kutokana na mvua kubwa, nilifadhaika sana na kuwaza kama kuna uwezekano wa kuruka.
Hahaha pole mkuu
Wazo lakuruka ndio huwa linakuja haraka vichwani mwa wasafiri wengi [emoji2]

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
Mimi napendekeza kwenye ndege kuwe na airbags zitakazokua na muundo kama wa nguo (overroll),

Hizo aibag zitakua kwenye muundo wa over rall na zitajifyatua na kua kama puto pale mtumiaji anakapovaa na kubofya kibatan kuruhusu ifanye hivyo. Hii itawekwa kwenye kila seat na itavaliwa na kila abiria wakati wa dharura.

Hiyo over roll itakua na accessories zote kama mtungi mdogo wa oxygen, gloves, mask n.k
 
Hakuna kifaa wala maelekezo unayo pewa kwenye ndege unaweza jiokoa ndege ikidondoka.
 
Bado kuna shughuli yakusogea mlangoni wakati ndege ikitikisika mkuu,, je abiria ataweza kuvaa kwa ukamilifu wakati ndege ikiyumba na yeye hana utulivu?

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…