Kwanini pilipili za mwendokasi zina bei ndogo ukilinganisha na aina nyingine sokoni?

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Kwa mliokwenda nchi za nje mfano bara la asia uwezi kuziona hizi pilipili za mwendokasi.

Mfano China ni walaji wazuri wa pilipili, ukikutana nao sokoni uwezi kuona wananunua hii jamii ya pilipili kwa jina mwendokasi. Wao hujikita na pilipili ambazo sio wageni tukiona kwenye mapishi yao na kuulizana zile pilipili si watashindwa chakula.

Lakini ni tofauti kabisa sababu ni kwamba ukali wake utofautiana na mwendokasi kuendana na ladha ya chakula pamoja na viungo.

Ila hii pilipili sasa ya mwendokasi ukiweka tu umeshavuruga chakula kabisa.
 
Aina zingine za bei ya juu ni zipi? Mbona pilipilo karibia zote bei ni ile ile ukiondoa pilipili hoho.
 
Aina zingine za bei ya juu ni zipi? Mbona pilipilo karibia zote bei ni ile ile ukiondoa pilipili hoho.
Hapana ndugu sio kila mazao yana fanana bei.Muulize aliyekuwaga mkuu wilaya iringa.
 
Zinastawi sana na kilimo chake ni chepesi
 
Si unasema pilipili sokoni neenda mabibo ujionee bei karibia zinafanana.
Embu nenda kisutu ukakute aina ya makabichi sio ulilozoea kila siku kukutana nalo kwenye msosi wako.
 
Embu nenda kisutu ukakute aina ya makabichi sio ulilozoea kila siku kukutana nalo kwenye msosi wako.
Lile ni soko la wahindi wengi wanalenga wahindi wanapigwa bei ya juu, we neenda Ilala au ma bibo soka la waswahili.
 
Lile ni soko la wahindi wengi wanalenga wahindi wanapigwa bei ya juu, we neenda Ilala au ma bibo soka la waswahili.
Nimekupeleka mbali kusutu nenda hapo mabibo kaulize Red cabbage .
kama inauzwa ovyo hapo mabibo si umesema vinafanana
 
Hujajibu swali langu, so naomba unijibu...

Hizo pilipili za mwendokasi zinalimwa wapi?
Swali ni kama uulize ndizi mzuzu ni za wapi mbona mi sijawahi kuziskia ...jibu lake ni zinalimwa kila sehemu hata uwani kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…