Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kwangu binafsi naona ni mwendelezo wa unafiki wa Polisi Tanzania. Umesikia hata siku moja pale inapotokea ajali ya gari za serikali, hasa hizi Landcruiser ST.. wakisema ajali imesababishwa na uzembe wa dereva? Na kila mtu anajua madereva wa hizi ST.. wanaendesha gari kwa fujo bila kufuata sheria au alama za barabarani. Lakini inapotokea wamepata ajali husikii hata siku moja Polisi wakisema ajali imetokana na uzembe wa dereva aliekuwa akienda spidi kubwa na kushindwa kuimiliki gari.
Na mbaya zaidi, madereva wa gari binafsi hata wakifa katika ajali, utasikia gari ilipinduka kwa sababu ya uzembe wa dereva, wakati hawajui hata nini kilitokea hadi ajali ikatokea. Mara nyingine dereva alikuwa anakwepa kumgonga mlevi au kugongana na dereva mpumbavu, lakini Polisi wanakimbilia kusema uzembe wa dereva utafikiri walishuhudia ajali ikitokea!
Angalia hii ajali ya hili Landcruiser la Mkuu wa Wilaya ya Seerenget. Na sisi raia tunasema ulikuwa ni uzembe wa dereva, tena akiwa na Mkuu wa Wilaya, kukimbiza gari hadi akashindwa kulimiliki na kupinduka na kuitia serikali hasara ya mamilioni ya fedha!