Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Uteuzi wa Emmanuel Nchimbi kuwa katibu mkuu wa CCM, kwa wanaokumbuka watu aliowapiga chini, walishangaa na kujiuliza kunani mteule wa Magufuli anawakumbatia aliowakataa aliyemtengeza?
Kabla ya vumbi kutua, akamchomoka Abdulrahman Kinana aliyedukuliwa akimsengenya na Nape na Makamba. Ghafla bin vuu, akamteua January Makamba waziri wa mambo ya nje.
Huku na huku tukaona waliokuwa wametemwa wakishika kani kuanzia Bashite hadi Nchimbi ambaye sasa ni mgombea mwenza. Je, imekuwaje waliokuwa wamekataa kwa usaliti wao wamerejeshwa? Je hii si kumsaliti aliyemtengeneza?
Je, walikuwa na bifu ambayo waliificha au ni usaliti uliokuwa umefichwa kwenye tabasamu, heshima na woga vya bandia mbali na kaunafiki? Mie wanangu sielewi.