Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Kumekuwa na watu wanaohoji kwanini rais anasifiwa sana ila hakosolewi.
Kwanza, ana mamlaka makubwa kikatiba. Anaweza kufanya lolote atakalo asivunje sheria. Mfano, alipomteua Makonda wengi walistuka na kulaumu lakini aliwapuuza.
Pili, alipomteua mkwewe na kumpa jukumu la kuchakachua, sorry kusimamia uchaguzi wengi wasiojua sheria wala kumtakia mema walilalamika.
Tatu, rais alirithi urais toka kwa mtangulizi wake aliyesifika kwa kupenda kusifiwa naye akarithi katabia hako. Hivyo, hana makosa maana huo ndiyo urathi wake toka kwa aliyemtengeneza.
Nne, katiba yetu ya hovyo alaumiwe Nyerere aliyeitumia kututawala kama mfalme mpaka alivyoshindwa kabisa akamuachia mzee Ruksa naye akaanzisha vijimchezo vyake kama kuendekeza udini, uholela uliozidishwa na Kikwete aliyerithi serikali yenye majivuno toka kwa Mkapa kabla ya kumkabidhi Magufuli aliyejigeuza mtetezi wa wanyonge na kutumia lugha hii kuendesha nchi Ki-Aminiamini au KiMseveniseveni kama siyo kiKagamekagame.
Mwisho, Tanzania ni kama maabara ya kufanyia kila majaribio.
Kama alivyowahi kusema mzee Mwinyi, ni kichwa cha mwendawazimu walevi kujifunzia kunyoa.