Kwanini refa alisimamisha shambulizi la Simba?

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Kuna kipindi Simba walishambulia Morison akampasia Kapombe na ilikuwa ndani ya 18 ,ilikuwa move ya goli. Naomba kufahamu kosa gani ilifanyika ,Tuache ile shuti ya Kanote halafu akapuliza offside.

Ila hata hivo hamna kelele baada ya mechi
 
Sababu nasikia kuna mchezaji wa UTO alikuwa kalala kwa maumivu uwanjani japo binafsi si kuona jambo kama hilo
 
Move ilizimwa kwa kupuliza filimbi wakati morrison anatuliza mpira kifulani. Refa alionesha ishara kuwa Morrison kaushika mpira. Filimbi ilitangulia kabla hata mpira haukumfikia Kapombe
 
Wanasema eti Morrison aliunawa!Ila ukiachana na yote,sikuona sababu ya Kibu kuendelea kuwepo uwanjani muda wote Huo wakati game ilimkataa!
Tukija Kwa Bocco ni vema tu akatafute ustaarabu mwingine timu nyingine,hata isingepigwa filimbi ya offside,tayari alishakosa goli Tena rebound amebaki na kipa!Derby ya kariakoo,dk ya 87 ubaoni 0-0 unakosa goli wakati kipa alishaanguka!
Ni wakati wa Tshabalala kupewa rasmi ukapteni mkuu!
 
kwakweli bocco hastahili kuwepo kwenye kikosi,kulenga goli ni ishu halafu kupoteza mipira na fouls zisizo za maana
 
Boko akubali tu kwamba jua limezama sema huyu Kibu naye awe anatokea benchi tu nguvu zimekuwa nyingi kupita akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…