Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Shalom wajumbe wa JF.
Mara tu baada ya kuingia madarakani 2015, Rais John Pombe Magufuli aliunda Kamati Maalum (ukipenda ita tume) ya kuchunguza mali za CCM nchi nzima. Kamati/Tume hii iliongozwa na Dk. Bashiru Ally.
Kamati hii ilifanya kazi kubwa na kuja na findings na mapendekezo ikiwa na kurasa 927 (kitabu). Bashiru alimkabidhi Mwenyekiti wa CCM Rais JPM huku Hamphrey Polepole akipewa nakala aliyopelekewa kupitia kwa Tito Magoti (sasa DC).
Ripoti ya Kamati hii ilibaini uchafu, madudu na kila aina ya ufisadi uliofanywq na uliokuwa ukiendelea kufanywa na makada wa CCM. JPM alitumia ripoti hii kama rungu kutaka atiiwe na kusujudiwa maana ulipoleta fyofyo uliitwa na kuoneshwa kurasa zinazokuhusu na kisha kuulizwa, "unanikubali tupotezee au unagoma twende Kisutu kwa kesi ya uhujumu uchumi?" Kwa woga wa makada wa CCM na hofu ya maisha ya gereza la Keko kila mmoja aliufyata mkia kasoro Bernard Membe.
Miongoni mwa waliofyata mikia yao ni pamoja na Nape aliyekutwa na wizi wa magari kadhaa ya chama yaliyotumika kwenye kampeni. January alikutwa na wizi wa 2.7 bilioni fedha za kampeni. Jengo la UVCCM lilimnasa Lowassa, Subhash Patel huku kina Rostam nao wakinasa kutaja kwa ufupi. Ni vigogo wachache sana walipona kwenye ripoti hiyo iliyofanya JPM aitwe mshamba.
Sitaki kuamini kwamba 4R za Samia ni pamoja na kuizika ripoti hii iliyogharimu mamilioni ya walipakodi kukusanywa. Sitaki kuamini kwamba Samia amefanya reconciliation na ufisadi na mafisadi. Na kama ni hivyo hilo litakuwa jambo baya sana na usaliti kwa umma.
Sumu hii ikiachwa itakiangamiza CCM 2025 maana utakuwa ni uchaguzi kati ya Ufisadi na Uadilifu. Rais Samia akiweka wazi ripoti hii na kuifanyia kazi kama mapendekezo yalivyo atajijengea heshima kubwa katika vita dhidi ya ufisadi. Lakini kama ataipotezea basi sidhani kama magari 160 ya maji ya washa-washa yaliyoagizwa kutoka Korea yatafua dafu 2025.
Rais Samia vaa ujasiri kuweka hadharani ripoti hii na kuifanyia kazi mapema. Kama umenyimwa hapo Ikulu usiione basi soon tutaitundika hapa hapa JF ili uisomee hapa. Kuwa JASIRI maana maadui zako wanataka kuifyatua kiasi kwamba nchi itatetemeka. Nishukuru baadaye.