Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Jaji Maarufu kimataifa Mhe. Joseph Sinde Warioba ameweka rekodi ya kipekee kwa kuongoza Tume mbili za Rais katika historia ya JMT na katika historia ya Majaji wa Tz. Tume yake ya kwanza ilikuwa ni ya kuchunguza kushamiri rushwa nchini; tume iliyoundwa na Mhe. Big Ben Mkapa ambayo hata baada ya kazi nzuri ya kiuweledi wa viwango vya juu iliyofanywa na Mwenyekiti Jaji Warioba bado utekelezaji wa ripoti ya Tume hiyo ulikuja kufanyika kwa kiwango cha chini sana huku washukiwa wachache sana akiwemo Mhe. Nalaila Kiula waziri wa ujenzi wakifikishwa mbele ya sheria. Tatizo ni Jaji Warioba mwenyewe? Au ni ripoti yake ni ngumu kutekelezeka? Au tatizo ni washauri wa mteuzi wake?Au tatizo ni mfumo wa uteuzi wa Tume hizi? Nadhani pana haja ya Wenyeviti na Makamishina wa Tume za Rais kuidhinishwa na Bunge kwanza ili kuhifadhi, kuendeleza na kuenzi heshima-tukuka za viongozi hawa kitaifa na kimataifa.
Tume ya pili aliyoongoza Mhe. Warioba ni ile ya Mabadiliko ya Katiba; iliyoundwa na Mhe. Kikwete ambayo nayo pia utekelezaji wake umekwama kwenye hatua ya Referendum baada ya Bunge Maalum la Katiba iliyoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kumaliza kazi yake. Je, tatizo ni Jaji Warioba mwenyewe? Au ni ripoti yake (rasimu ya pili) iliyokuja kudurusiwa na Bunge Maalum la Katiba kutotekelezeka? Au tatizo ni washauri wa mteuzi wake? Au tatizo ni mfumo wa uteuzi wa Tume hizi? Nadhani pana haja ya Wenyeviti na Makamishina wa Tume za Rais kuidhinishwa na Bunge kwanza ili kuhifadhi, kuendeleza na kuenzi heshima-tukuka za viongozi hawa kitaifa na kimataifa.
Tume zote mbili hizi nyeti sana zinazochagiza mustakabali na hatma ya nchi na zinazohusu agenda-mahsusi zimegharimu taifa rasilimali-fedha nyingi kiasi kwamba kutotekelezeka ripoti zake kunaashiria kiwango cha juu cha unafiki, ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka. Mwenendo huu usioeleweka unamuweka Jaji Warioba katika mazingira tata ya kumpunguzia heshima yake katika jamii za kitaifa na kimataifa.
Aidha, madai ya Jaji Warioba ya Katiba mpya yanaegemea kwenye rasimu yake ya pili aliyowasilisha kwa Rais (iliyobeba maoni ya wananchi) na Rais kuiwasilisha Bunge Maalum la Katiba au yanaegemea kwenye rasimu ya Bunge Maalum la Katiba? Jaji Warioba aweke wazi madai yake yanaegemea wapi kati ya rasimu mbili hizi.
Duru za wachunguzi wa medani za siasa na maendeleo zinadhihirisha kukwama kwazo kujuwa kama labda ripoti hizi za Jaji Warioba na msimamo wake usioyumba huenda zinamchumia faraka na warasimu walio na maslahi binafsi kwenye masuala haya yanayochagiza uchunguzi wa kitume!
Kama hali ndiyo hii je, taifa limuache Jaji Warioba apumzike kwa heshima asiteuliwe kwenye Tume au uteuzi uwao wote ule labda hizo za kimataifa tu? Au liamue kuanzia sasa kutekeleza retroactively ripoti zote hizo mbili ili kuondoa hisia za unafiki, ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka?
Jaji Warioba Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tz akiwa kwenye moja ya mijadala ya Tume hiyo ambayo ni zao la madai ya Karatasi Nyeupe (White Paper).
Jaji Maarufu kimataifa mwenye ithibati ya UN kwa weledi wake Joseph Sinde Warioba, ambaye pia aliwahikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa JMT na Waziri Mkuu Mstaafu, Mwanasheria Mkuu wa JMT, Jaji wa Mahakama ya EAC, Jaji wa UN kwa masuala ya mazingira ya baharini na Mwenyekiti wa Tume mbili za Rais za Rushwa (Mkapa) na Mabadiliko ya Katiba (Kikwete) akiokolewa na wasamaria wema kufuatia kushambuliwa na kada wa chama Paulo Makonda kwa tofauti za kimawazo na maoni juu ya agenda ya taifa. Taswira zote kwa hisani ya google.