Kwanini Samsung wameanza kukomaa na processor za Mediatek?

Prince Nadheem

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2012
Posts
1,259
Reaction score
1,056
Habari za leo wajamvi?

Kama heading invyosema hapo juu. kwa sasa Samsung mobile phones zinaonekana kutoa mid range budget phones kwa kasi sana kila leo ili kuendana na makampuni ya simu ya kichina. Kwa upande wa makampuni ya simu ya kichina nao wameonekana kuja juu kwa kuweka specifications bora zaidi na zaidi na hata kwa performance na kuanza kuwa tishio kwa samsung kwa soko la simu za mkononi za Android.

Mfano wa simu zifanyazo vizuri kwa sasa hasa kwenye masoko ya Africa, India, Pakistan, Latin America etc ni:
-Xiaomi
-Oppo
-Vivo
-Huawei
-ZTE etc.

Sasa katika hoja ya msingi, Samsung kwa segment ya budget phones alianza kwa kuweka chipset za Exynos au snapdragon ambazo ni nzuri hasa katika simu zake za A10, A20, A20s, A20e N.K.

Sasa hivi karibuni kaanza kuharibu kwa kuweka Helio MTK processor kwa simu zake kama vile A10s, A21, A12 N.K

Sasa nimeangalia nikaona kabisa kuwa Samsung anaanza kupotezwa na hawa jamaa wa China kwa maana baadhi ya makampuni wanatumia processor za Exynos na Snapdragon na ni simu za kwenye the same category na pricewise Samsung bado anakuwa yupo juu kidogo. Na pia hizi kampuni za simu za kichina zinatoa decent specs hata upande wa storage.

Mfano simu kama Oppo A53 na Vivo Y20 zinatumia chipset ya exynos na storage ya 64GB/3-4 Gb RAM. Kwa upande wa Samsung simu ya category hiyo ni Samsung A12 (MTK Helio, 32/3 GB minimum). Sasa hii imekaaje kwenu wataalamu kwa Sammy kuanza hizo MTK and selling at a higher price kuliko ilivyotakiwa iwe?

Karibuni sana kwa michango yenu
Cc: CHIEF MKWAWA
 
Habari za leo wajamvi?

Kama heading invyosema hapo juu. kwa sasa Samsung mobile phones zinaonekana kutoa mid range budget phones kwa kasi sana kila leo ili kuendana na makampuni ya simu ya kichina. Kwa upande wa makampuni ya simu ya kichina nao wameonekana kuja juu kwa kuweka specifications bora zaidi na zaidi na hata kwa performance na kuanza kuwa tishio kwa samsung kwa soko la simu za mkononi za Android...
Wao samsung wana Target soko, na soko linaendana na bei ndogo na wateja ndio wanaoamua. Katika soko la simu ni wateja wachache tu ndio wanaomudu kutoa pesa kwaajili ya Flagship. Wengi wanataka Budget phone na wengineo midrange.

Sasa matumizi ya Mediatek kwa budget phone ndio yenyewe ingawa Mediatek nao wanajiweza na sio processor mbaya kama miaka iliyopita.

Pamoja na matumizi ya mediatek kwa samsung, bado wanajua namna ya kucheza na soko na wateja wao. Kuna vitu kama display, RAM, Battery optimization, uhakika wa updates n.k hivyo ni baadhi ya vitu vinavyofanya waendelee kubaki sokoni.

Kwa maoni yangu hapa , samsung hawajafanya jambo baya. Kwani mediatek sio processor mbaya haswa kwa budget na midrange phone hivyo bado samsung wamechukua hatua njema.
 
Wao samsung wana Target soko, na soko linaendana na bei ndogo na wateja ndio wanaoamua. Katika soko la simu ni wateja wachache tu ndio wanaomudu kutoa pesa kwaajili ya Flagship. Wengi wanataka Budget phone na wengineo midrange...
Nimepata Jambo Jipya Sasa Hivi
Kuhusu Samsung
Mkuu
Hebu Niongezee Madini Kwenye Hii
Samsung Galaxy S6 SM ~ G920F
Hii Hapa Tanzania Kwenye Network Itakuwa Sawa Maana Ninayo
Ndiyo Nataka Niifanyie Setting!
 
Wao samsung wana Target soko, na soko linaendana na bei ndogo na wateja ndio wanaoamua. Katika soko la simu ni wateja wachache tu ndio wanaomudu kutoa pesa kwaajili ya Flagship. Wengi wanataka Budget phone na wengineo midrange.

Sasa matumizi ya Mediatek kwa budget phone ndio yenyewe ingawa Mediatek nao wanajiweza na sio processor mbaya kama miaka iliyopita.

Pamoja na matumizi ya mediatek kwa samsung, bado wanajua namna ya kucheza na soko na wateja wao. Kuna vitu kama display, RAM, Battery optimization, uhakika wa updates n.k hivyo ni baadhi ya vitu vinavyofanya waendelee kubaki sokoni.

Kwa maoni yangu hapa , samsung hawajafanya jambo baya. Kwani mediatek sio processor mbaya haswa kwa budget na midrange phone hivyo bado samsung wamechukua hatua njema.
Bado kuna vitu kama display bado amedowngrade sana Samsung. Sasa hivi kwa baadhi ya simu za mid range zinanyimwa hata protection. Kwa mfano simu kama Samsung A12 haina screen protection; wakati Oppo, Xiaomi, Vivo na ZTE za kundi hilo hilo la mid range phone wanatoa hata Corning gorilla Class 3 etc. Bado pia GPU katumia PowerEVR.
Sasa ukijumlisha hayo yote pia simu inakuwa nzito (bulky) mkononi ukiishika ikilinganishwa na washindani wake.
The only winning point kwa Samsung na quad camera za 48MP japo hazina uwezo wa kuzoom in ikiwa kwa hiyo mode.
Tuendelee na mjadala wetu ymollel
 
Nimepata Jambo Jipya Sasa Hivi
Kuhusu Samsung
Mkuu
Hebu Niongezee Madini Kwenye Hii
Samsung Galaxy S6 SM ~ G920F
Hii Hapa Tanzania Kwenye Network Itakuwa Sawa Maana Ninayo
Ndiyo Nataka Niifanyie Setting!
Kuna demand kubwa ya processors kiasi kwamba kwa sasa kuna deficit kwenye soko.
Vifaa vya electronic na magari vinahitaji processors wakati suppliers hawakidhi demand.
Hapo hapo TSMC ana wafavour apple kuliko wengine.
 
Bado kuna vitu kama display bado amedowngrade sana Samsung. Sasa hivi kwa baadhi ya simu za mid range zinanyimwa hata protection. Kwa mfano simu kama Samsung A12 haina screen protection; wakati Oppo, Xiaomi, Vivo na ZTE za kundi hilo hilo la mid range phone wanatoa hata Corning gorilla Class 3 etc. Bado pia GPU katumia PowerEVR.
Sasa ukijumlisha hayo yote pia simu inakuwa nzito (bulky) mkononi ukiishika ikilinganishwa na washindani wake.
The only winning point kwa Samsung na quad camera za 48MP japo hazina uwezo wa kuzoom in ikiwa kwa hiyo mode.
Tuendelee na mjadala wetu ymollel
Mkuu Jibu rahisi ni kwamba samsung hatengenezi low end mwenyewe, Anaetengeneza simu za Xiaomi na Samsung ni kampuni moja huko China inaitwa Wing tech, zinatengenezwa Kisha zinapigwa tu label hii Samsung hii Xiaomi.

Hivyo ni vyema kuangalia kwa umakini specs kabla hujanunua.

Kuhusu mediatek zipo nzuri, kuna Helio G series na dimensity series wana soc za maana humo, ila vipo vimeo pia P series kama hio A12 inatumia soc za Jamii ya kina Tecno.
 
Yaani leo kwa mara ya kwanza umekubali kuwa kuna mediatek nzuri. 👍

Kuhusu kutengenezewa simu hilo swala lipo na ni la kawaida kabisa kwenye maswala ya tech (Outsourcing). Kwenye OEM kinachoangaliwa na mmiliki ni kukidhi vigezo na masharti ya mkataba. Ukirudi nyuma kidogo utagundua hata Blackberry zilikuwa zinatengenezwa na kampuni ya TCL, Nokia ni HMD Global.

Kifupi samsung sasa wamekubali kushindana na wapinzani wao ambao kampuni zingine zimewapuuzia uwepo wao ambapo kibiashara ni mtego mbaya sana.
 
Bado kuna vitu kama display bado amedowngrade sana Samsung. Sasa hivi kwa baadhi ya simu za mid range zinanyimwa hata protection. Kwa mfano simu kama Samsung A12 haina screen protection; wakati Oppo, Xiaomi, Vivo na ZTE za kundi hilo hilo la mid range phone wanatoa hata Corning gorilla Class 3 etc. Bado pia GPU katumia PowerEVR.
Sasa ukijumlisha hayo yote pia simu inakuwa nzito (bulky) mkononi ukiishika ikilinganishwa na washindani wake.
The only winning point kwa Samsung na quad camera za 48MP japo hazina uwezo wa kuzoom in ikiwa kwa hiyo mode.
Tuendelee na mjadala wetu ymollel

Kweli Ni vitu vingi samsung ameondoa ili kufanya simu bei rahisi na uzalishaji rahisi kwa wingi. Simu nyingi ametoa AMOLED display ameweka LCD. Build Quality nayo ni ya kawaida ni plastic zaidi, simu zinafanana fanana ubunifu umepungua pia.
 
Yaani leo kwa mara ya kwanza umekubali kuwa kuna mediatek nzuri. 👍

Kuhusu kutengenezewa simu hilo swala lipo na ni la kawaida kabisa kwenye maswala ya tech (Outsourcing). Kwenye OEM kinachoangaliwa na mmiliki ni kukidhi vigezo na masharti ya mkataba. Ukirudi nyuma kidogo utagundua hata Blackberry zilikuwa zinatengenezwa na kampuni ya TCL, Nokia ni HMD Global.

Kifupi samsung sasa wamekubali kushindana na wapinzani wao ambao kampuni zingine zimewapuuzia uwepo wao ambapo kibiashara ni mtego mbaya sana.
Sijawahi kukataa kuhusu mediatek as a soc toka G na Dimensity zitoke, most of time mada kama hizi huja pamoja na Tecno, maana mpaka leo Tecno Sidhani kama kuna hata moja Inayokuja na Dimensity, zipo chache za G series kama G70 nazo pia zipo overpriced.
 
Samsung kapigwa na Apple kwenye flagship phones , Kwa hiyo sasa inabidi abanane na wachina na njia rahisi ndo hiyo kutengeneza simu inferior ili aendelee kuuza pia Kwa bei ndogo . Kifupi kanyosha mikono juu kakubali yaishe .
 
uzushi huu s21 series inauza vizuri na wametangaza result za Q1 wameingiza faida kubwa tu na driving factor ni s21.

ukitoa Nchi zinazouza simu kwa mikataba nchi kubwa kama Usa, Japan etc, sehemu zote watu wanaonunua simu rejareja Samsung anamkimbiza Iphone, mfano mzuri ulaya.

na akiuza Iphone pia Samsung anaingiza faida ya maana tu hivyo kwake ni win win
 
nawewe huwa una ushabiki maandazi sana.

kwani apple kutoa matoleo 4 bei na sifa tofauti kwa mwaka ni baada ya kupigwa na nani!!!!!
 
uzushi huu s21 series inauza vizuri na wametangaza result za Q1 wameingiza faida kubwa tu na driving factor ni s21.

ukitoa Nchi zinazouza simu kwa mikataba nchi kubwa kama Usa, Japan etc, sehemu zote watu wanaonunua simu rejareja Samsung anamkimbiza Iphone, mfano mzuri ulaya.

na akiuza Iphone pia Samsung anaingiza faida ya maana tu hivyo kwake ni win win

Fuatilia record za mauzo ya simu za Samsung Kwa miaka mitatu minne iliyopita. Angalia ni wapi wanauza zaidi . Pia nenda most sold flagship Samsung humkuti au ni kwa tabu sana . Ndo maana nikasema soko lao kubwa limebaki kwenye simu za kawaida .

Sijaongelea mambo ya Faida maana kama ni Faida Apple hana mpinzani Kwa hiyo tusiguse huko .
 
Back
Top Bottom