Kwanini Serikali haijengi Techinical College Kanda ya Ziwa badala yake wanarundika vyuo vyote Dodoma?

Yaani Nyerere miaka 25 madarakani ilishindwa hata kujenga chuo kikuu huko musoma! Na musoma pasingekuwa pamepoa hivyo kama pangekuwa na chuo kikuu!
Nyerere simlaumu sana maana kwa sera zake za ujamaa sioni shida sana. Shida iko kwa watendaji.

Ukiangalia kanda ya ziwa imetoa mawaziri, viongozi wakubwa sana nchi hii lakini hawajapakumbuka kwao.

Musoma mji umepoa sana aisee.
 
Haya matusi Sasa haya mkale mlimani city sisi tumegoma kuwapikia

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nyerere alikuwa anaangalia maendeleo kwa tanzania nzima. Sio kanda ya ziwa tu.
Hata kwao kwenyewe hakujajengeka saana maana alikuwa na vision tofauti
 
Haya matusi Sasa haya mkale mlimani city sisi tumegoma kuwapikia

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kwan cafeteria za chuo hakuna.
Wanachuo hawawahitaji Bali ni wenyeji tu na umaskini wao.

Mimi sionagi faida ya chuo mahali zaidi ya kuongeza umalaya sehemu,muingiliano wa watu na magonjwa.

Ishu ni kuwa na wasomi wengi na wenye hela pia
 
Nyerere simlaumu sana maana kwa sera zake za ujamaa sioni shida sana. Shida iko kwa watendaji.

Ukiangalia kanda ya ziwa imetoa mawaziri, viongozi wakubwa sana nchi hii lakini hawajapakumbuka kwao.

Musoma mji umepoa sana aisee.
Yaani ukifika musoma hutamani hata kuwekeza yaani pamepoa ndo maana watu wa mara wamewekeza sana mwanza!
 
Mngemshauri yule msukuma wenu awajengee mwanza tech badala ya kujenga chatto I A na burigi.
 
Mtu wenu jiwe alikuwa Rais alishindwa nini kuwajengea hizo technical college Matokeo yake akaenda jenga uwanja wa ndege huko chato maporini, mara lihospital kubwa na kusahau mwanza ka ndio mji mkubwa kanda ya ziwa, so jilaumuni wenyewe
 
Mbona unajibu kwa hasira sana?
 
Vyuo vijengwe kusini kwa Tanzania kumesahaulika kwa makusudi sana
 
si kweli mkuu, tusiingie kwenye mtego huu.
 
Kuna vyuo vikuu vingapi nchi hii? Je kila mkoa kipo?
Usirukie kila mkoa wakat mtoa mada kasemea kwa kanda nzima ya ziwa hakuna kikuu cha serikali, kila mkoa serikali yako inaweza kujenga maana vilivyopo
kanda ya pwani udsm,sua,ardhi,mzumbe.
Katikati ya nchi udom.
Nyanda za juu kusini kuna MUST.
Kaskazini kuna ATC.
Kanda ya ziwa kuna PRiVATE cha SAUT.
 
Watu wananiona kama napendelea kanda ya ziwa kwenye maada hii! Ila naangalia population,economic power ya kanda ya ziwa alafu chuo kikuu cha serkali hamna hii haiko sawa!
 
Zilikuwepo technical colleges 4, Dar es salaam, Arusha, Mbeya na Karume Zanzibar. Mbeya na Dar zilisha badirishwa hadhi, sjui kuhusu hizo mbili. Mwanza kuna tawi la DIT, lakini nahisi unaufahamu mdogo kuhusu mfumo wa elimu ya ufundi na uhandisi.
 
Mkuu nasema sawa kilicho badilishwa ni mbeya kuwa MIST na vyuo hivi vinatoa technicians wenye diploma japokuwa saiz zinatoa degree pia! Usifikir mi sijui so technical college sio vocational training college! Hicho cha mwanza ni branch ya DIT haijawa na course za kutosha nahakijapanuliwa pia na ndo ninachohoji hapa!
 
kuna mji unaitwa Chato kanda ya ziwa, waliwezeshwa kuwa na technical collage, ama ujenzi haujakamilishwa
Ile likuwa inajengwa VETA sio Tecnical College. Fungu lilihamishwa toka upanuzi wa CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TABORA ili kuwa chuo kikuu, na kuhamishiwa Chato. Tabora walijenga ghorofa moja tu na mradi ukasimama.
 
Kusini Mtwara,Lindi na Ruvuma Kuna chuo gani au nao sio Watanzania?
Magharibi pia Kuna chuo kipi?
Ninyi watanzania wa Kanda ya ziwa, Pwani na kaskazini ndio mnajikuta watanzania zaidi ya wenzenu au sio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…