Kwanini Serikali haikatazi kufuga mjini lakini inakataza kulima?

Kwanini Serikali haikatazi kufuga mjini lakini inakataza kulima?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Watanzania huwa tuna mambo ya ajabu sana. Tupo kinyumenyume sana. Kulima mazao kama mahindi mjini hakuna madhara yoyote, zaidi zaidi ni faida kwa mazingira ya mjini. Ni kama bustani mjini. Lakini utakuta miji mingi inasheria ya kutoruhusu mazao kama mahindi kupandwa mjini, wakitishia kuyakata.

Wanatoa sababu za wezi na kupendezesha mji. Sababu zisizo na mashiko yoyote. Maana mimea inafanya mji iwe mizuri na mjini hakuna mashamba ya kusema yatakuwa makazi ya wezi.

Lakini serikali hiyohiyo inaruhusu ufugaji wa kuku, ng'ombe, nguruwe, bata na mbuzi mjini. Hawa ni hatari sana kwa afya na mazingira. Wanasababisha harufu, wanaeneza magonjwa(hii ni hatari kubwa sana) na kuchafua mazingira.

Kwanini tunafikiri kinyume nyume? Kwanini hatupigi marufuku ufugaji mjini?
 
Nakazia hapa ufagi mjini ni kero sana jamani hata kama ndo kuongeza kipato ni kero kwa wengine kero kubwa mnoooo , mbolea wakianza kuchoma Moshi unaturudia , harufu ya kinyesi cha wanyama mmmh jamn serikali hiingilie kati jamani , hatuwaonei wivu jamani wenye mifugo yenu.
 
Back
Top Bottom