Raphael Mtui
Member
- Nov 26, 2024
- 78
- 204
Karibu kila mtu amewahi kujiuliza swali hili.
Kwa nini serikali isi-print fedha nyingi na kuwagawia wananchi ili waondokane na umasikini?
Ni kweli, kila nchi ina uhuru wa kuamua ichapishe kiasi gani cha fedha na kukiingiza kwenye uchumi, ama tuite mizunguko ya fedha.
Lakini kama tunataka uchumi ufe leo leo, basi serikali ichapishe mapesa mengi na kuyaingiza kwenye mzunguko!
Ngoja tukufafanulie: Iko hivi; kinachofanya mtu aulize swali hili ni pale tu anapodhani ukuaji wa uchumi ni mabunda ya pesa kuwa mitaani.
Iko hivi: noti nyingi sio ukuaji wa uchumi hata kidogo. Yaani, pesa sio uchumi, wala sio utajiri, bali pesa ni kitu kinachosaidia tu kubadilisha bidhaa.
Sasa sikia: kama nchi ikitaka kuwa tajiri kwa ku-print hela nyingi na kuziruhusu ziingie mtaani, kuna mabalaa mawili:
La kwanza ni hyper-inflation, yaani mfumko mkubwa wa bei unaoweza kuporomosha uchumi kabisa.
Tuna nchi tatu duniani zilizowahi kufanya hili jambo.
Ujerumani, Venezuela na Zimbabwe.
Mwaka 2018, Venezuela walichapisha mihela, haraka nchi ikazama kwenye hyper-inflation. Mfano, kuku wa shilingi 5000 alipanda bei akauzwa milioni 15!
Mwaka 2008 hapo Zimbabwe, mabunda ya pesa yalichapishwa, mshahara wa mwalimu ukafika matrilioni kwa mwezi, lakini bei ya mkate pekee ikawa bilioni 300!
Bei ya pipi ikawa dola za Zimbabwe milioni 231!
Mwaka 1923 Ujerumani ilichanganyikiwa, wafanyakazi wakaongezewa mishara yao maradufu lakini haikufua dafu!
Ikawa balaa pale Ujerumani.
Swali ni kwa nini kuchapisha pesa nyingi kusababishe mfumuko wa bei?
Ni rahisi mno! Fikiri hapo ulipo una elfu hamsini pekee, kisha ukapewa milioni mia nane sasa hivi: Jambo la kwanza utakalofanya ni shopping. Utahakikisha unanunua kila ulichotamani siku nyingi!
Fikiri watu wote nchini wakagawiwa mapesa kama wewe. Kila mtu atakimbilia manunuzi.
Sasa, kinachofuata kwa haraka ni nini? Ni mfumko wa bei! Vitu vitapanda bei vibaya mno!
Kwa nini vipande bei? Kwa sababu kila mtu anakimbilia madukani kufanya manunuzi. Kila mtu amepewa 'purchasing power'. Kila mtu amekuwa mteja. Kila mtu yupo njiani kwenda kununua.
Bidhaa ni zile zile, ila pesa zimeprintiwa nyingi kuliko uzalishaji wa bidhaa na huduma za nchi husika. Puuuuu! Mfumuko wa bei utakaoporomosha kabisa uchumi!
Lakini usisahau, bidhaa zikipanda bei ni nini kinafuata? Thamani ya pesa kushuka haraka, kiasi ambacho watu hawatataka hata kuitumia.
Ngoja nikupe mfano: kuna mikate milioni mbili nchini nzima. Kila mkate unauzwa 1000. Mikate yote ni sh. bilioni mbili.
Ila nchi ikaprint mapesa mengi kupitiliza na kuyaingiza mitaani. Matokeo yake, watu wakaanza kununua mikate hadi wale waliokuwa wakichemsha viazi wanavyolima shambani kwao watatamani wabadilishe mlo.
Hata wale waliokuwa wakinunua mkate mmoja watataka kununua mikate kumi. Baada ya saa chache, mikate haitauzwa tena sh 1000 mkate mmoja utauzwa 100,000!
Wafanyakazi wataandamana kutaka mishara iongezwe, kila mahali itakuwa ni fujo, nchi haitatawalika, kisa ni nini, serikali imeprint hela nyingi na kuziingiza kwenye mzunguko.
Uchumi kukua ni nini? Sio mabunda ya pesa! Mabunda ya pesa ni kujidanganya kuwa ni uchumi umekua.
Kumbe uchumi kukua ni pale tu uzalishaji wa bidhaa na huduma utakapoongezeka, sio nje ya hapo hata kidogo!
Ndio maana serikali huchapisha pesa kiwango cha asilimia 2-3 tu ya pato la ndani, yaani GDP.
Raphael Mtui 0762731869