Kwanini Serikali ilituficha kuugua kwa Dkt. Magufuli?

Ila jamani si aliutangazia umma?
Labda swali liwe kwa nini alichelewa kutangaza. Au kwanini hakuutangazia umma kwamba Rais ni mgonjwa na amelazwa
 
Hata akiulizwa atasema tu kwamba taarifa zilizotolewa na serikali zilikuwa sahihi. Ni kweli serikali yetu haiwajibiki kwa mengi. Naamini hatua sahihi ni sote tuungane tudai Katiba mpya kuanzia na Rasimu ya Warioba. Hapo angalau tutapata kigingi cha kuwawajibisha viongozi wetu
 
Taarifa gani sahihi zilizotolewa na serikali?
 
Taarifa gani sahihi zilizotolewa na serikali?
Zote.. alizotoa Majaliwa, na alizotoa yeye Samia. Kwa nature ya nchi yetu, si rahisi hata waandishi wetu kukusanya ujasiri wa kumbana mama Samia kwenye kona.

Si unakumbuka Pasco Mayala mwenyewe aliwahi kukiri hapa JF kwamba baada ya kuuliza swali la Katiba kwa Magufuli, biashara zake zikayumba sana. Kwaiyo usitarajie mwandishi wa habari mtanzania aulize hayo.

Kikeke mwenyewe alishindwa kumbana Samia pamoja fursa nyingi za follow up questions zilizojitokeza. Si kwamba Kikeke hana data. No. Anaangalia USTAWI wake atakaporejea nchini hivi karibuni baada ya kustaafu BBC.

Labda mimi na wewe tuwe wana habari, urejee nchini, tuombe press na tumbane kisawasawa.
 
Kabla ya 17/03/2021, Haikuwa serikali yake bali ya Magufuli. Kwahiyo aliyeandaa utaratibu wote wa kuficha taarifa zake za ugonjwa alikuwa mwenda zake mwenyewe. Na hii haikuwa mara ya kwanza kwa Magu kuficha taarifa za afya yake.

Ni kama mara mbili au tatu kusikika kwa tetesi kuwa ni mgonjwa na yeye kutoonekana kwa muda lakini baadae alikuwa anaibukia kanisani au Chato.Bahati mbaya safari hii ikaishia kwa yeye kwenda kwa muumba wake.

Hivyo sioni kuwa ni swali la msingi kuulizwa SASHA, kwani huo ndo ulikuwa utaratibu wa serikali ya JPM.
 
Speaking someone who agreed on everything the deceased did!!
Get outta here.
 
Inawezekana walificha wakiwa na tumaini kuu kwamba atarejea ktk hali yake(kuondoa taharuki) na bahati mbaya haikuwa walivyodhani.
Basi hili ni funzo kwa viongozi wetu kuwa wawazi pengine maombi ya wengi yangewezafanya kitu.
R.I.P JPM
 
Kwa mujibu wa katiba ya URT,kifungu na ibara sikumbuki wataalamu wa katiba waje hapa kusaidia,endapo raisi wa nchi hii ataugua na atakuwa Yu mahututi hajitambui kwa kipindi cha wiki mbili,inabidi makamu wa raisi aapishwe kuwa raisi, kutoka na maelezo hayo ndiyo sababu inayopelekea taarifa za kuugua kiongozi mkuu zisiwe wazi,ili angalau kukwepa hicho kifungu na kusubiri kudra za mwenyezi,mgonjwa aweze kupona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…