sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
KWANINI SERIKALI IMEKUWA KIMYA SANA KWA WAZEE WA SIMBA NA YANGA.
Tumetoka mbali sana na timu zetu za Simba na Yanga,kiumri ni sawa na timu hizi kuwa babu sisi wajukuu,timu zimeanzishwa miaka 1930's mpaka kufikia hapa si suala dogo.
Kwa miaka ya karibuni, kumeibuka wimbi la wapinga Maendele ambao hujiinua na kujifanya wanamiliki na hizi timu,kuliko mtu yeyote, hali inayo zorotesha maendeleo ya soka nchini .
Tumeona serikali kupitia BMT ikinyamazia sintofahamu hizi, ilihali ikifurahia mafanikio ya vilabu hivi kimataifa, wakati ikishindwa kuziunga mkono juhudi kufikia kilele cha mafanikio katika changamoto na figisu wanazo kumbana nazo.
Hizi si timu za mtaani, ni timu za wanachama zilizoko kihalali kwa mujibu wa sheria ya usajili wa vilabu vya michezo. Lakini mbali na kuwa vilabu vya michezo vinabaki kuwa taasisi ambazo zitakuwa za kibiashara zitakazo ingizia mapato serikali.
Kwa kuwa timu hizi zipo kisheria na mlezi wao ni Baraza La Michezo la Taifa, na kwa kuwa kufikia hatua ya kuzifanya kampuni hupitia mchakato wa vikao vya wanachama kwa mujibu wa katiba zao na sheria zilizowekwa na serikali, kwanini linapotokea suala la Kilomoni na Akilimali serikali inarudi nyuma.
Nasema Uakilimali na Ukilomoni umekuwa unakua kwa kasi na kurudisha nyuma sera ya michezo nchini ilihali serikali ipo kimya.
Tumeona viongozi wa vilabu wako magereza kwa kesi za utakatishaji pesa, lakini wahujumu uchumi wa mali za vilabu wenye kung'ang'ania hatimiliki za majengo wapo nje wanatembea. Hii si sawa katika misingi ya utawala bora.
Leo taifa linanufaika kwa maamuzi ya wanachama kukubali kuifanya club kuwa kampuni,uwakilishi wetu kimataifa umeongezeka, tumefungua wigo mpana wa utalii na uwekezaji nchini kupitia mpira, iweje mtu mmoja au kikundi kimoja kiturudishe kwa kuhodhi maazimio ya wengi.
Waziri mwenye dhamana ya michezo, chonde chonde, hatuna nafasi ya kupigania hatimiliki, tunataka hili suala liwekwe kisheria kwa maslahi mapana ya nchi zetu, tumechoka kubadilishana migogoro ya majungu kila mwaka kwa maslahi binafsi. Hizi ni timu za wananchi ziendeshwe kwa mujibu wa sheria na kanuni.