Kwanini Serikali inamkalia kimya Mr Kuku anavyoanzisha utapeli mpya kwa Watanzania?

J33

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
1,552
Reaction score
1,513
Suala la Mr Kuku na utapeli aliyowafanyoa Watanzania unajulikana wazi na imejadiliwa sana hapa JamiiForums.

Huyu jamaa alikamatwa na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na baadae akakiri na kuipa Serikali bilioni tano ajabu ni kwamba baada ya kutoka mahabusu aliendelea na biashara ile ile na sasa ameanza mradi mwingine wa kilimo cha mahindi ambao uelekeo wake ni ule ule kwamba unawapa 1.2M then kwa mwaka unapata 5M.

Ina maana serikali hailioni hili?

Je, hii ni mbinu ya baadae kumfungulia tena kesi na kuchukua mabilion ya Watanzania?

Sio jukumu la Serikali kuwalinda Watanzania?
 
Anajuwa atavuwa samaki wengi na kuwapa 10% dola, wanajuwa, wanamwacha avune kwanza
 
Kama wewe mwenyewe huwezi kwenda shamba na muda huna ukimpa hiyo 1.2M na mwaka ukiisha anakupa 5M kuna shida gani? cha muhimu kuwe na legal documents.

Me naona kijana anatumia akili kwa kuzichanga karata zake vizuri, hapo ni kama mnamkusanyia mtaji na sio lazima alime kuwalipa inawezekana hata akafanya dili lingine akapiga superprofit akawalipa na yeye akabaki na mkwanja.
 
Ona hii
Screenshot_20211109-075901.jpg
 
Utawala umebadilika

Enzi zile alkua jiwe, sahivi tuko kwa mama wa RUKSA

Ni mwendo wa shamba la bibi
 
Kama wewe mwenyewe huwezi kwenda shamba na muda huna ukimpa hiyo 1.2M na mwaka ukiisha anakupa 5M kuna shida gani? cha muhimu kuwe na legal documents.

Me naona kijana anatumia akili kwa kuzichanga karata zake vizuri, hapo ni kama mnamkusanyia mtaji na sio lazima alime kuwalipa inawezekana hata akafanya dili lingine akapiga superprofit akawalipa na yeye akabaki na mkwanja.
Makubaliano yoyote kwa huo mradi ni batili!
 
Hii ni kama anauza shares katika shughuli za kilimo, lakini hiyo faida siyo ya uhalisia kabisa. Atapata wapi faida baada ya miezi mitatu wakati kuotesha mahindi mpaka kuvuna inachukua zaidi ya muda huo? Halafu atakuwa analima misimu mingapi kwa mwaka? Jee anayo insurance ya kilimo pale ambapo kitafeli?

Haya ndiyo yanatakiwa ayatolee maelezo ya kuridhisha kwanza, otherwise huu ni utapeli wa aina nyingine.
 
Niliona juzi kapost picha yupo kitandani, baada ya kuanguka na pikipiki, anapenda sana ma mbio na lile tuku tuku lake.
 
Suala la Mr Kuku na utapeli aliyowafanyoa Watanzania unajulikana wazi na imejadiliwa sana hapa JamiiForums.

Huyu jamaa alikamatwa na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na baadae akakiri na kuipa Serikali bilioni tano ajabu ni kwamba baada ya kutoka mahabusu aliendelea na biashara ile ile na sasa ameanza mradi mwingine wa kilimo cha mahindi ambao uelekeo wake ni ule ule kwamba unawapa 1.2M then kwa mwaka unapata 5M.

Ina maana serikali hailioni hili?

Je, hii ni mbinu ya baadae kumfungulia tena kesi na kuchukua mabilion ya Watanzania?

Sio jukumu la Serikali kuwalinda Watanzania?

Kutakuwa Hakuna sheria anavunja
 
Back
Top Bottom