Nakazia kama babyfancyWaache wapenda mserereko
Makubaliano yoyote kwa huo mradi ni batili!Kama wewe mwenyewe huwezi kwenda shamba na muda huna ukimpa hiyo 1.2M na mwaka ukiisha anakupa 5M kuna shida gani? cha muhimu kuwe na legal documents.
Me naona kijana anatumia akili kwa kuzichanga karata zake vizuri, hapo ni kama mnamkusanyia mtaji na sio lazima alime kuwalipa inawezekana hata akafanya dili lingine akapiga superprofit akawalipa na yeye akabaki na mkwanja.
Hii ni kama anauza shares katika shughuli za kilimo, lakini hiyo faida siyo ya uhalisia kabisa. Atapata wapi faida baada ya miezi mitatu wakati kuotesha mahindi mpaka kuvuna inachukua zaidi ya muda huo? Halafu atakuwa analima misimu mingapi kwa mwaka? Jee anayo insurance ya kilimo pale ambapo kitafeli?
Suala la Mr Kuku na utapeli aliyowafanyoa Watanzania unajulikana wazi na imejadiliwa sana hapa JamiiForums.
Huyu jamaa alikamatwa na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na baadae akakiri na kuipa Serikali bilioni tano ajabu ni kwamba baada ya kutoka mahabusu aliendelea na biashara ile ile na sasa ameanza mradi mwingine wa kilimo cha mahindi ambao uelekeo wake ni ule ule kwamba unawapa 1.2M then kwa mwaka unapata 5M.
Ina maana serikali hailioni hili?
Je, hii ni mbinu ya baadae kumfungulia tena kesi na kuchukua mabilion ya Watanzania?
Sio jukumu la Serikali kuwalinda Watanzania?