Kwanini serikali isitenge muda wa kutosha kwa walimu kufundishwa mtaala mpya

Benaya123

New Member
Joined
Jan 13, 2024
Posts
1
Reaction score
3
Naona Wizara ya Elimu kushirikiana na TAMISEMI wanaendelea kufanya maboresho kwa walimu juu ya uelewa na utekelezaji wa mtaala mpya ulioletwa.

Shida yangu iko pahala, Maafisa Elimu ngazi za mikoa na wilaya wao walipitia mtaala huu kwa semina wezeshi takribani kw asiku 5, baadae wakafuata viongozi wa walimu ngazi ya Kata ambao ni Maafisa Elimu kata.

SASA HIVI kila kona ya nchi walimu wametumia siku moja hadi mbili kupitishwa katika mtaala huu mpya.

Hoja yangu kwa wahusika Tamisemi na Wizara ya Elimu kuona umuhimu wa kutenga muda mwafaka... rasilimali pesa ili hawa waliju wanaotekeleza mtaala huo wapate mafunzo/semina na wapate muda mrefu kupitia vipengele hivyo na sio kuwabuluza.
NAWASALIMU KWA JINA LA J.M.T.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…