Kwanini Serikali isitoe bei elekezi ya gesi za majumbani?

Kwanini Serikali isitoe bei elekezi ya gesi za majumbani?

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Habari za leo ndugu wananchi, wiki chache zilizopita kumetokea mfumuko wa bei kwenye mafuta na gas.

Hivi ni kwanini serikali isitoe bei elekezi katika mitungi ya Gas kama inavyofanya kwenye mafuta ili tujue sababu za mfumuko huu wakutisha?

Maana kwenye mafuta walitwambia sababu sio wao bali ni soko la dunia, sasa kwenye gas wanatwambiaje?

Mkoa ninaoishi gas mtungi mkubwa wa kg 15 ilikuwa sh 48,000/= unaletewa mpaka nyumbani, badae wakafika 49,000/= tukaona ni kawaida, badae wakafika 53,000/= tukaanza kugugumia sasa imefika 58,000/= tukiendelea kuwachekea huenda wakaongeza na ka 2000/= kabisa iwe 60,000/=

Kwanini Serikali isitwambie changamoto ni nini? Au inataka turudi kwenye mkaa?
 
Serikali ya SSH ilishazungumza kitambo sana, kuwa tatizo ni mfumuko wa bei kwenye soko la dunia, wewe ulikua wap??
 
Kwani ukuelewa somo pindi ccm wanasema mmeipenda wenyewe, chaguo lenu wenyewe. Wacha muisome namba.

Ila walitoa tangazo la upandaji wa bei kati 1000-10000
 
"Acha waisome namba eeeh, watasoma namba CCM mbele kwa mbele" namba ndo zinasomwa ivo. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukienda na kadi ya ccm tena ya kielektroiki unauziwa kwa sh 31,500.

Wanaoumia kwa bei hizo ni chadema, cuf na zitto co ltd
 
Kwenye mafuta ilisema hivyo kwenye gas nakumbuka walisema wao Hawahusiki
Mwanzoni walisema hawahusiki lakin mwisho wa siku walituweka bayana kuwa shida ni bei kupanda katika soko la dunia fuatilia, thread hyo iko humu, na tulihoji sana kuwa inawezekanaje gas inayopatikana humu Tz ilete athari katika soko la Dunia!!

FUATILIA MAMBO NDUGU
 
Jana nilikuwa sehemu nasindikiza weekend.
Mara simu inaita toka nyumban nikaambiwa gase imekata . Napita kuuliza mtungi mdogo 24000/= ilibidi nirud home maana no stimu tena.
Maisha magumu sana
 
Back
Top Bottom