Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Wachumi njoo mnisaidie kitu hapa.
Mimi ni mtumishi kwenye shirika moja la maendeleo, na mshahara wangu ni Milioni 2 na laki 8 ila kutokana na sheria na taratibu za nchi ninatakiwa nilipe PAYE kiasi cha 668000, hapo ninabakiza kiasi cha 2,132,000 hivi kiasi ambacho bado ninahitakija kulipa bima yangu ya NHIF bila kusahau makato ya pensheni. Hii pesa sio kwamba napewa mkononi bali inapita kwenye mfumo wa benki, binafsi natumia huduma za benki ya CRDB ambapo ili kutoa kiasi hiki inabidi kukatwa tena kodi pamoja na tozo za serikali.

Nina watoto watatu ambao wapo shule, inanihitaji kuwalipia ada zao za shule ila bado tena nikilipia kwa kutumia akauntiyangu wanakata kodi nyingine na tozo. Sio hilo tu, mimi sio mtu wa kutembea na pesa, ni rahisi kutembea na kadi ya benki na kufanya malipo kwa wepesi ila nikununua bidhaa bado kodi wanachukua.
Nikitaka kuwapatia wazee wangu pesa ya kula kuku na kufurahia matunda ya elimu na uchapakazi wangu tena bado wanachukua kodi! Najiuliza kwa sauti ya kinyonge je, kwenye hii 2,132,000 ambayo imetoka kwenye 2,800,000 je serikali haiwezi kuchukua PAYE halafu mambo yakaendelea? Ni vitu ambayo ukivitazama vinaumiza sana.
"Swali kwa wachumi na wadau wa maendeleo, Je hakuna namna bora ya kuchukua kodi bila kumchachafya mwananchi?"