Kwanini Serikalini inasema haikuchoma soko la Karume huku ripoti ya tume haijatoka?

Kwanini Serikalini inasema haikuchoma soko la Karume huku ripoti ya tume haijatoka?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Soko la Karume limeungua na Serikali imeunda tume na imetoa siku 14 tume itoe majibu ya uchunguzi wake.

Kabla ya tume kutoa majibu tayari tumeanza kusikia Serikali ikikana kuhusika kuchoma moto.

Kama haitoshi tumeanza kusikia eti mateja ndio wamechoma moto.

Je, kwanini Serikali inasema haihusiki kabla ya tume?

Kwanini tunaambiwa mateja ndio wamechoma kabla ya tume?

Nilitarajia kama Serikali haihusiki ingesema hayo kwenye tume.

Na kama ni mateja wamechoma yangesemwa hayo kwenye tume ili taarifa ya tume ndio tuisikie.

1642572752866.jpg
 
Pengine najiuliza kwa nini machinga walitaka wajenge wenyewe soko lao . Huenda kuna msiri aliwatonya ya kuwa mwekezaji ameandaliwa. Hii siyo haki ikiwa uvumi wa kuwa atawekwa mwekezaji katika soko la Karume. Inauma mpaka nashindwa niandikeje
 
Soko la Karume limeungua na Serikali imeunda tume na imetoa siku 14 tume itoe majibu ya uchunguzi wake.

Kabla ya tume kutoa majibu tayari tumeanza kusikia Serikali ikikana kuhusika kuchoma moto.

Kama haitoshi tumeanza kusikia eti mateja ndio wamechoma moto.

Je, kwanini Serikali inasema haihusiki kabla ya tume?

Kwanini tunaambiwa mateja ndio wamechoma kabla ya tume?

Nilitarajia kama Serikali haihusiki ingesema hayo kwenye tume.

Na kama ni mateja wamechoma yangesemwa hayo kwenye tume ili taarifa ya tume ndio tuisikie.

Khee!

IMG_20220113_105213.jpg
 
"tumepata mwekezaji atajenga maghorofa ya kutosha kwenda angani...Hawa ndugu ZETU tutawatafutia eneo lingine wafanye biashara bila bughudha,hii sirikali NI ya watu wanyonge"

Hizi ndoto AISEE acha TU niote
 
Kile kifungu cha sheria kinachosema kwamba,ardhi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ni Mali ya serikali ikiwa chini ya dhamana ya raisi wa jamhuri,naona kifungu hicho awamu hii kinafanyiwa kazi sana,kwamba raisi anayo mamlaka ya kubadili matumizi ya ardhi kwenda matumizi mengine,kifungu hicho kitatafuna sana raia wa kawaida na kueaacha wakiwa hohe hahe.
 
Back
Top Bottom