Kwanini sherehe za harusi hazilipiwi TRA wakati ni pesa za umma?

Kwanini sherehe za harusi hazilipiwi TRA wakati ni pesa za umma?

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
2,567
Reaction score
416
Wakuu ni hoja ndogo hapa;

Eti kwanini pesa za sherehe kama, harusi, send off na kitchen party hazilipiwi kodi TRA? Wakati pesa zake zinachangiwa na watu/umma?

Ni pesa za umma hizo, why?
 
wakuu ni hoja ndogo hapa eti kwa nini pesa za sherehe kama,harusi,send off na kitchen party hazilipiwi kodi TRA? wakati pesa zake zinachangiwa na watu /umma? ni pesa za umma hizo,why?

Unajua maana ya Public Funds wewe
 
TRA wanatoza kodi mapato yanayokuwa faida, sio matumizi.

mkuu una uhakika kuwa hizi pesa za harusi hazina faida? kwani hivyo vinywaji mnavyokunywa si vimenunuliwa na serikali si inapata faida kupitia hivyo vitu? ujui kila kitu unachokula katika sherehe kimelipiwa ushuru katika manunuzi yake ndio maana kuna ushuru wa vinywaji,vyakula na vilevi, so umekubali kwamba serikali inapata faida kupitia pesa za sherehe kama harusi
 
Kodi si inalipwa kutokana na huduma mbalimbali kama chakula,MC nk.Sasa kama TRA hawakusanyi huko basi kuna shida
 
Harusi sio biashara, bali wanaotohuduma katika hizo harusi ndio wanafanya biashara na hao ndio wanatozwa kodi.Harusi haijirudii bali watoa huduma katika maharusi wataendelea na biashara yao na hao ndio wanapaswa kulipa kodi.
 
Fedha za umma zinatokana na makusanyo ya kodi, ushuru na ada mbali mbali lakini sio michango! Ukisema michango ya sherehe itozwe kodi basi ujue hata ya misiba itafutata. Kuchangia maendeleo au suala lingine kutokana na michango ya sherehe ni hiari ya wachangaji hawapaswi kulazimishwa. Mimi nakumbuka wakati nahitimu darasa la 7 siku hiyo hiyo ya sherehe tuko kuandaa mapochopocho mwaka 1978 ndipo tulipoona wakimbizi waliokimbia uvamizi wa majeshi ya Idd Amin wa Uganda. Walimu walitueleza kuhusu hali ya hao watu na njaa ya kutembea mwendo mrefu bila kula kitu. Kwa kauli moja tuliamua kuwaachia chakula cha sherehe sisi hatukula. Lakini tukifanya hivyo kwa hiari yetu bila kushurutishwa.
 
Wakuu ni hoja ndogo hapa;

Eti kwanini pesa za sherehe kama, harusi, send off na kitchen party hazilipiwi kodi TRA? Wakati pesa zake zinachangiwa na watu/umma?

Ni pesa za umma hizo, why?


Kuna uzi humu utafute uusome.
 
Back
Top Bottom