Kwanini sherehe za Uhuru huwa tunaonesha mambo ya kijeshi zaidi badala ya uchumi na uhuru wa kimaendeleo?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Nimefunguliwa akili na wanaharakati flani wa Iran wakiipa changamoto serikali yao. Wanadai Janga la korona limekwanyua uchumi wa nchi yao lakini katika sherehe za kitaifa wao wanaonyesha mambomu mapya waliyoyabuni badala ya maonyesho ya vile ambavyo serikali imefanya kuwaondoa katika wimbi la umasikini.

Badala ya maonyesho yetu ya uhuru kujikita kwenye judo na magwaride ziongezwe package nyingine show za kiuchumi ambazo zitasaidia watu wapate hamasa za kiuchumi.

Maana uhuru tulioupata sio kutoka katika ukandamizwaji wa kijeshi na kikoloni tu bali hata ukombozi wa kifikra na kiuchumi.

SIku hiyo kungekuwa na maonyesho angalau hata ya wanasayansi wetu bora, watu waliofanya mambo makubwa kimaendeleo nchini, na ubunifu mwingine utakaoambatana na ubunifu wa kijeshi.

Maoni...
 
Bado miaka minne tuingie kwenye uchaguzi lakini watu wanapanga mipango ya kampeni

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Hata mm niliwaza hilo sana !!! Eti wakati was sherehe tunaoneshwa jw wakipasua tofali kwa kichwa!?? Pathetic!?
Maendeleo ya viwanda technolojia hawaoneshi
 
zile ni sherehe zilizoandaliwa na jeshi,kilimo na uchumi ni 7 7.

kama unataka maonyesho hayo siku hiyo kaongee na wanajeshi ktk ratiba za siku hiyo.
 
nilikuwa sijui. Kumbe ni sherehe yao
 
Nimefunguliwa akili na wanaharakati flani wa Iran wakiipa changamoto serikali yao. Wanadai Janga la korona limekwanyua uchumi wa nchi yao lakini katika sherehe za kitaifa wao wanaonyesha mambomu mapya waliyoyabuni badala ya maonyesho ya vile ambavyo serikali imefanya kuwaondoa katika wimbi la umasikini.

Badala ya maonyesho yetu ya uhuru kujikita kwenye judo na magwaride ziongezwe package nyingine show za kiuchumi ambazo zitasaidia watu wapate hamasa za kiuchumi.

Maana uhuru tulioupata sio kutoka katika ukandamizwaji wa kijeshi na kikoloni tu bali hata ukombozi wa kifikra na kiuchumi.

SIku hiyo kungekuwa na maonyesho angalau hata ya wanasayansi wetu bora, watu waliofanya mambo makubwa kimaendeleo nchini, na ubunifu mwingine utakaoambatana na ubunifu wa kijeshi.

Maoni...
Wanaharakati ni masikini always
 
Mkuu mkorinto Wanajeshi wa Tanzania ndio walioleta Uhuru? Lini ilikuwa?

mkuu jeshi lina maana kubwa sana hasa katika neno husika "UHURU"

lakini kama nilivyotangulia kusema hawana hati milikina sherehe husika,ndio maana watoto wa halaiki nao wana maonyesho yao siku ile.

so kama unaona una jambo la maana kuonyesha taifa siku ile,ni kuwasiliana nao tu wajue wanakupa ratiba ipi.
 
Mambo ya uhuru na uchumi ni siku ya mlipo kodi...
 
Back
Top Bottom