Kwanini Shukuru Kawambwa anazuia mitihani isifanyike Ijumaa na Jumamosi?

tpmazembe

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
2,469
Reaction score
586
Nashangaa kwa nini Huyu mtu anaiburuza hii wizara kiasi hicho? mbona hao wakristo na waislam wakiwa na shuguli zao za kawaida tu huku mtu haijalishi siku muda wote utawaona wakiruka ruka.

wabudha wanasali asali alhamis basi na alhamisi azuie, wakrito wengine husali jpili na jtano nazo zizuiwe kufanywa mitihani, kama ni mitihani ifanyike jtatu na jnne tu.

Huyu waziri anatakuwa kujua utanzania ni zaidi ya uislam na ukristo, huwezi endesha ofisi za umma kwa idiology za kidini ni kuharibu taifa.

Akina mkwawa,kinjekitile,mangi ,isike ambao ni wazee wetu walipiginia taifa hili kabla hata kufikiwa na hizo dini.Utawala huu wa awamu ya nne umekuwa kituko sana hasa kutokea viongozi ambao ni religious minded people badala ya watu wanaojali utaifa.
 
Kwani usipofanyika Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kuna tatizo gani?Na kama issue kwako ni muda basi kwanin hujasema pia jumapili?au mitihani itafanyika jumapili?

Na bado hili la uchaguzi mkuu kufanyika jumapili inabidi libadilishwe, linasababisha wananchi wengine washindwe kupiga kura hasa sehemu ambazo kuna foleni kubwa.

Tuna siku saba kwa wiki, kwenye uamuzi wowote, tuangalianeni kama wana wa nchi, hapa ni kwetu na hii ni ncgi yetu, tuchukuliane pamoja.
 

tatizo ni kwamba hiyo jpili bado inafanyika na hawajazuia , alafu kuna dini zingine kama wabudha siku yao ya ibada ni alhamis , wengine jtano
 
tatizo ni kwamba hiyo jpili bado inafanyika na hawajazuia , alafu kuna dini zingine kama wabudha siku yao ya ibada ni alhamis , wengine jtano

Hivi Wabudha ni asilimia ngapi ya Watanzania?yawezekana ata unaposoma hawapo.Lazima tukubali tu kuna majority kwenye lolote.Kumbuka demokrasia sio kumpa kila mtu anachotaka bali kuwapa wengi wanachotaka.

Kama kigezo ni ibada, basi na jumapili ilipaswa mtihani usifanyike.

Na ningefurahi kwani ningepata muda wa siku hizo kujiandaa vizuri na mitihani inayokuja mbele.
 
Huyu kawambwa hivi degree alimpa nani.. Yan anaongoza wizara kwa upepo... Sasa mambo ya udin yanahusu nn ujinga huu
 

kama ni kuangalia majority basi hata mitihani ikifanyika kila siku wahakikishe kwanzia saa sita na nusu inakuwa imeisha mpaka saa saba unusu na saa sita unusu isiwepo mpaka saa kumi na robo maana mida hiyo kila siku ni ya ibada kwa waislam
 

what's wrong of u guy?
i think u ar not okey!
 
ndio maana tanzania haiendelei. maana excuses haziishi.
 
viongozi wa ccm wanaamua wanavyotaka wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…