Kwanini si Dkt. Ali Hassan Mwinyi?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Nafuatilia msiba wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Watu wengi wamemzungumzia. Mengi yamesemwa juu yake.

Lakini moja ambalo nimeliona limekosekana ni ule utambulisho wa Dkt.!

Katika maisha yake yote ya uongozi, Rais Mwinyi hakuwahi kupewa shahada ya udaktari wa heshima kama ilivyokuwa kwa aliyemtangulia na waliokuja nyuma yake?

Sijawahi kuona wala kusikia popote pale Rais Mwinyi akitambulishwa kama Dkt. Ali Hassan Mwinyi.

Hiyo ni kwa nini? Hakupewa hiyo shahada ya heshima? Alipewa hiyo shahada ya heshima lakini kwa vile hakuwa mpenda makuu, hakuona umuhimu wa kuutanguliza huo utambulisho na hivyo kuwafanya watu wengine nao kutokumtambulisha kwa huo utambulisho?

Au hatambulishwi hivyo kwa sababu watu walio wengi hawajui kama alipewa hiyo shahada ya heshima?

Najua marais Nyerere na Mkapa walikuwa na hizo shahada za heshima lakini ilikuwa ni nadra sana kusikia au kuona Dkt. Julius Nyerere au Dkt. Benjamin Mkapa.

Ila kuanzia Kikwete kuja mpaka hivi sasa, kila mtu ni Dkt. so and so……
 
Mkuu ukiwa nacho au ukiwa na uwezo nacho huoni umuhimu wake, ukiwa unajua huna uwezo wa kukipata au kukifikia ndio shida huanzia hapo, unaqeza mlima mtu barua ya kumfuta kazi kisa hajaanza na neno Dr.
 
Marehemu MWINYI hakutaka MAKUU kama hawe wengine
 
Hayati Mwinyi na hao wenzake wawili uliowataja hawakuwa na "njaa" ya "kutofautishwa". Sijaamanisha pia kwamba wengine wana hiyo njaa!
 
Ungeanza kwa kuuliza hiyo trend ya kugawa udaktari wa heshima kama njugu ulianzaje, na kwanini media hatimaye zilishindwa kutofautisha kati ya udaktari wa kusomea na udaktari wa heshima, na udaktari wa kusomea vyuo halisi aka brick and mortar institutions na udaktari wa mitandaoni..
 
Sasa hivi Dr ni swala la kisiasa na uchawa, leo nimesikia hata shekh mkuu wa bakwata akiitwa Dr sijui kasoma lini na wapi
 
hao walielewa taratibu za Vyuo Vikuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…